WABUNIFU wametakiwa kujua jinsi ya kulinda bunifu zao kwa kutumia mihimili ya miliki bunifu ikiwa ni pamoja na kujua nyenzo wanazoweza kuzitumia, hatua na aina gani ya miliki bunifu zinazohitajika kwa bunifu zao.

Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Judith Kadege alisema Tume hiyo ipo kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwashauri wadau tofauti katika sekta ya utafiti na ubunifu nchini.

Alisititiza kuwa, elimu ya miliki bunifu inasaidia kujua haki za wabunifu kabla ya kuanza kubuni kitu ambacho wanakifikiria, pia hapo alipobuni akitaka teknolojia hiyo au bunifu yake itumike sehemu nyingine anatakiwa afanya kitu kipi kabla.

“Yote hayo tunafundisha ili kulinda ile miliki bunifu yake isije ikaibiwa, au ikatupwa au ikatumiwa ndivyo sivyo bila ya idhini yake ama kibiashara au kwa matumizi mengine,” alisema.

Kwa maelezo yake wabunifu wengi wana mlengo wa ujasiriamali kwa hiyo kwenye kusaidia hizo teknolojia zao katika mlengo wa kujua haki zao za ulinzi wa miliki bunifu itasaidia kujua wapeleke wapi bunifu ambayo imepata ulinzi wa miliki bunifu ili iweze kufanyiwa kazi.

“Hii inafanyika duniani kote kuwa ulinzi wa miliki bunifu unakupa wewe mmiliki wa hiyo bunifu uwezo wa kuweza kujua jinsi gani unaweza kuongea hata na makampuni makubwa waweze kutumia hiyo teknolojia yako,” alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia katika Tume hiyo, Dkt.Athuman Mgumia alisema waliandaa mafunzo hayo kwa wabunifu 60 walioshiriki na kushinda Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) ili kuendeleza bunifu zao.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia katika kuboresha teknolojia zao na kuweza kuhakikisha kama zinawafikia walengwa wao waliowakusudia.

Mhandisi wa Mitambo ambaye ni mbunifu Kennedy Mwakatundu, alikiri kuwa kama wabunifu kuna vitu ambavyo hawavilindi kisheria au sheria haiwalindi hivyo kupitia mafunzo hayo kutawawezesha kuwa na ujuzi wa kulinda kazi zao.

“Kuna wakati ambapo migogoro inaweza kutokea lakini kumbe inaweza kuepukika bila matatizo yoyote na watu kupelekana hatua zingine, kama mbunifu unatakiwa kuelewa jinsi ya kuepuka hiyo migogoro ili usipotezewe muda wa kuihangaikia,” alisema.

Mbunifu huyo ambaye ametengeneza mashine ya kusafisha fukwe za bahari ambazo hali yake siyo nzuri alishauri mafunzo hayo pia yawe ni sehemu ya kuwaandaa watoto wadogo kuweza kujua ikiwa wana kipaji fulani na kama akikitumia kipaji alichonacho kitamnufaishaje na nani atakuwa mlinzi wake.

Mbunifu mwingine wa kitanda cha kuweka kwenye gari la wagonjwa ambachokinajiendesha chenyewe, Diana Kaijage alisema mafunzo waliyoyapata yatawasaidia katika kulinda kazi zao walizozifanya.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendeleshaji na Uhaulishaji wa Teknolojia (COSTECH) Dkt.Athuman Mgumia katika akieleza waandishi wa habari lengo la mafunzo hayo.
 Mshauri wa masuala ya mambo ya hakimiliki bunifu, kutoka Kituo cha uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Judith Kadege akifafanua juu ya umuhimu wa haki miliki bunifu. 
 Wa kwanza kulia ni mbunifu wa kitanda cha kuweka kwenye gari la wagonjwa ambachokinajiendesha chenyewe, Mhandisi Diana Kaijageakizungumzia kuhusiana na kitnda hicho katika magari.
 Wa pili kushoto ni Mhandisi Kennedy Mwakatundu Mbunifu ambaye ametengeneza mashine ya kusafisha fukwe za bahari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi alivyotengeneza mashine ya kusafishia fukwe za bahari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...