Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka  King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua na kuziba tundu la moyo wa mtoto kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto 33 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa bila kufungua kifua ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na  wenzao kutoka  King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia  mtoto upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kurekebisha mishipa ya damu ya moyo  katika  kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya watoto 23 wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...