Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais menejimenti na utumishi wa Umma Kapteni John Mkuchika ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  kudhibiti vitendo vya rushwa katika Vyama vya Ushirika kutokana na ubadhilifu unaofanywa na wafanyakazi.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuchika wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru wenye kaulimbiu ya kupambana na rushwa ni wajibu wa kila mtu uliofanyika jijini hapa.

Mhe Mkuchika amesema, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na TAKUKURU lakini bado yapo malalamiko mengi ya wakulima kutolipwa kwa wakati, ikiwemo kudaiwa rushwa ili waweze kulipwa, fedha zao ambazo ni haki yao.

"Vyama kupokea fedha na kutowalipa kabisa baadhi ya wakulima, ni ukosefu wa uadilifu kwa viongozi na watumishi wa Vyama vya Ushirika ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali ambazo sio halali,'amesema Mkuchika..


Amesema TAKUKURU mnapaswa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki ili Vyama vya Ushirika visiwe ni kichaka cha wala rushwa,wezi na wala rushwa za haki ya wakulima.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa katika Vyama vya Ushirika, wapo baadhi ya wafanyakazi wamejilimbikizia mali ambazo wanashindwa kuzitolea maelezo ya jinsi walivyozipata, hivyo ameitaka TAKUKURU kuchukua hatua stahiki na kuwasilisha mapendekezo ya nini kifanyike.

Aidha, Mhe Mkuchika ameipongeza TAKUKURU kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 950 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa Wilayani Ruangwa Oktoba, 2019 ya kuitaka TAKUKURU kufuatilia fedha zote walizodhulumiwa wakulima wa ufuta mkoani Lindi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Generali  John Mbungo amesema katika tathmini ya utendaji  wao mwaka huu wamefanikiwa kwa asilimia 88.1 kitu ambacho ni kiwango cha juu kuwahi kufikia.

Amesema kutokana na agizo la Rais Dk John Magufuli la kukusanya fedha za wakulima wa ufuta zilizoibiwa na vyama vya ushirika wamefanikiwa kukusanya sh zaidi ya million 900 ambazo zitakabidhiwa kwa wakulima.

Amesema awali Rais Magufuli amesema wakulima hao waliibiwa sh million 423 na vyama 10 vya ushirika,lakini katika uchunguzi wa Takukuru wamebaini sh billion 1.43 ambazo zimeibiwa na vyama 31 vya ushirika.

“Tumebaini ni vyama 31 vya ushirika na fedha zilizoibiwa ni zaidi y sh billion moja na hadi sasa milioni 900 tayari zimereshwa na zilizosalia zitarejeshwa zote kwa sababu tarehe ya mwisho ni leo," Amesema Mbungo.

Mbali na hilo amesema jumla ya miradi 1,106 katika sekta ya maji,elimu,Afya na ujenzi ambayo inathamani y ash Trion 1.5,katika ufuatiliaji wao kiasi cha sh billion 43.3 kimebainika kufanyiwa ubadhilifu na hatua stahiki dhidi ya wahusika zinaendelea kuchukuliwa.

Amesema sh billion 23.7 zimeokolewa kutokana na oparesheni mbalimbali za uchunguzi na uzuiaji rushwa na kuongeza kuwa mali zenye thamani y ash billion 10.1 zilizopatikana kwa njia ya rushwa zimetaifishwa na mali za washtakiwa zenye thamani y ash billion 25.27 na Dola za Marekani million 5.67ziliwekewa zuio kwa lengo la ukamilishaji wa taratibu za kisheria kwa ajili ya utaifishaji wake.

Mbali na hilo alisema katika utekelezaji wake kesi 497 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini,zikiwemo rushwa kubwa nne zilizofunguliwa katika mahakama ya mafisadi nchini,ambapo kati ya hizo wameshinda kesi  206 ambapo ni sawa na asilimia 60.4 jambo ambalo ni mafanikio makubwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika ,akizungumza wakati  akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika jijini Dodoma leo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo akitoa taarifa ya utekelezaji ya TAKUKURU Wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliofanyika  jijini Dodoma leo

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...