NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
KATIKA
kukabiliana na wimbi la baadhi ya wenyeviti wa mitaa na vitongoji
kuhusishwa na migogoro ya ardhi na rushwa wenyeviti wapya
waliochaguliwa katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa katika
halmashauri ya Mji Kibaha, mkoani Pwani ,wamekemewa kujihusisha na
vitendo hivyo ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya serikali yao.
Aidha
wameaswa kuendelea kusimamia sheria ndogo iliyowekwa kuhusu muda wa
kuruhusiwa kucheza pool na kunywa pombe kuwa ni saa kumi jioni na ambae
atakiuka sheria hiyo na mwenye baa wote wakamatwe.
Hayo
aliyasema mkuu wa wilaya ya kibaha Assumpter Mshama wakati wa mafunzo
ya kuwajengea uwezo wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa hao ambayo
yameandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelazaji wa
majukumu yao ikiwemo kuweka mikakati ya kupambana na migogoro ya ardhi
pamoja na rushwa.
Alielezea
kipindi cha nyuma wenyeviti wa mitaa walisumbua kuwa chanzo cha kuuza
ardhi mara mbilimbili na wengine kusababisha migogoro ya ardhi isiyo na
tija .
"Baadhi ya
wenyeviti wa mitaa walichangia kuongeza changamoto ya migogoro ya
ardhi,sasa msiende kuwa vinara wa kufanya waliyokuwa wakifanya wengine"
Assumpter
alieleza,pia kilichowatokea wapinzani wa vyama vingine na kuacha
kugombea uchaguzi wa serikali za mitaa ingekuwa vyema wakasusia na
uchaguzi mkuu ujao, kuanzia kwa madiwani na wabunge ili CCM imalize kazi
.
"CCM imeshajiimarisha
kuanzia ngazi ya chini,ni chama gani kina mipango mizuri kama hii,yaani
unakuta chama kina viongozi kuanzia kata tuu,wanakula wakubwa
wanashindwa kujiimarisha kuanzia chini,na CCM tutaendelea na mwendo
uleule tutashinda kwa kishindo"alifafanua Assumpter.
Nae
mwenyekiti wa mtaa wa Msangani mwajuma makuka alisema wamepokea mafunzo
yote waliyopewa juu ya majukumu yao na atakwenda kuyasimamia ikiwemo
suala la elimu hasa kutatua changamoto za kielimu.
Wakati
huo huo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Kibaha Jennifer Omolo
alieleza lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kuweza kuwaongezea ujuzi
na uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao katika kuwasimamia
wanannchi.
Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi ,Kibaha Mjini Maulid Bundala alisema wenyeviti wa
mitaa wanawajibu wa kusimamia na kutatua changamoto za wananchi kabla ya
kufika ngazi ya juu na wanapaswa kusimamia utekelezaji wa ilani ya
chama hicho bila kulegalega.
Mafunzo
hayo yamewashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe 438
ambapo kati yao wenyeviti ni 73 pamoja na wajumbe wake 365 kutoka
katika halmashauri ya mji Kibaha na kushirikishwa viongozi mbali mbali
wa serikali .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...