Kampuni ya kutengeneza Mabasi aina ya Yutong imetoa mafunzo kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji nchini, namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi katika mabasi hayo yanayofanya safari zake mikoani na nje ya nchi ili kuweza kujikinga pindi yanapopata hitilafu na kuwaka moto lengo ikiwa ni kupunguza ajali za moto.

Mafunzo hayo  ya siku mbili yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yamefunguliwa  leo na Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi,Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Fikiri Salla huku washiriki hao wakifundishwa nadharia na vitendo katika kudhibiti majanga ya moto na ikiwa pamoja na kuangalia mifumo ya magari hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Naibu Kamishna Fikiri alisema sasa ni wakati wa sayansi na teknolojia na jeshi halina budi kuanza kujifunza njia mbalimbali za udhibiti wa majanga kwa kutumia teknolojia huku akiishukuru kampuni ya Yutong kwa mafunzo hayo.

“Tunapitia kipindi cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia naamini mafunzo haya yatawawezesha askari wetu kujifunza njia hizo za kisasa sambamba na kuelewa mfumo mzima wa mabasi hayo ambayo yamekua mengi hivi sasa hapa nchini na yakitumika katika usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali” alisema Naibu Kamishna Fikiri

Aidha mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong wakiongozwa na Meneja Huduma wa Kampuni hiyo, Lang Chang Ling,Mtaalamu wa Usalama kwenye gari,Ma Jiong  na Mhandisi wa Huduma, Zhao Le Hui

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili walisema wanaamini baada ya mafunzo kumalizika watakua wamepata elimu ambayo itawaongezea kitu katika shughuli zao za kila siku zinazohusiana na majanga ya moto na uokoaji.
 Mkuu wa Kitengo cha Usalama,Majanga ya Moto na Uchunguzi Naibu Kamishna Fikiri Salla, akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji(hawapo pichani), wakati akifungua mafunzo ya namna mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasi aina ya Yutong. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, Jijini Dodoma yakiendeshwa na Wakufunzi kutoka Kampuni ya kutengeneza mabasi aina ya Yutong.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Mkufunzi  kutoka Kampuni ya Mabasi ya Yutong Lang Chang Ling akitoa ufafanuzi jinsi mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto inavyofanya kazi kwenye mabasihayo  kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini  katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma ,leo ambapo mafunzo hayo ya siku mbili yameanza.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...