Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess  alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona  kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu kutoka  JKCI,  Israel na Ujerumani. Kushoto ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini Ujerumani Felix Berger.

Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess  akizungumza na mama wa mtoto aliyefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja wa  kuziba tundu la moyo katika  kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani.
Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani alipotembelea JKCI  kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo. Katika kambi hiyo watoto 55 walifanyiwa uchunguzi wa moyo, kati ya hao 18 walifanyiwa upasuaji mdogo wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba, saba watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi na 30 watatibiwa hapa nchini.
 
 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini Ujerumani Felix Berger akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess jinsi tundu la moyo linavyozibwa kwa njia ya upasuaji mdogo wa moyo kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto  inayofanywa na wataalamu kutoka  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess  na wataalamu wa afya kutoja JKCI, Ujerumani na Israel mara baada ya balozi huyo kumaliza ziara yake ya  kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu kutoka  JKCI,  Israel na Ujerumani. Katika kambi hiyo watoto 55 walifanyiwa uchunguzi wa moyo, kati ya hao 18 walifanyiwa upasuaji mdogo wa kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba, saba watapelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi na 30 watatibiwa hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...