Mcheza basketball nyota wa Marekani Kobe Bean Bryant (August 23, 1978 – January 26, 2020), amefariki dunia katika ajali ya helikopta huko California mapema leo, imethibitishwa.
 Mchezaji nyota huyo wa Basketball ambaye katika Maisha yake yote ya uchezaji ya miaka 20 alichezea Los Angeles Lakers ya NBA, amefariki na watu wengine wane kwenye ajali hiyo, eneo la Calabasas mjini Los Angeles, jimbo la California. Chanzo za ajali bado kinachunguzwa.
 Aliingia katika NBA moja kwa moja akitokea shule na kushinda ubingwa wa NBA akiwa na na Lakers mara tano.
 Kobe alikuwa mchezaji katika timu ya magwiji wa NBA mara 18, na mara 12 katika timu ya All-Defensive na pia Mchezaji Bora MVP mwaka 2008.
 Akiaminika kuwa mmoja wa wacheza basketball bora wa muda wote, aliongoza kwa kuwa mfungaji bora kwa misimu miwili, na alikuwa mfungaji bora wa nne katika ligi zote na mchezaji pekee katika nafasi ya Guard aliyecheza misimu 20 mfululizo.
 
 Sehemu ya Tukio
Kobe na familia yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...