Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

KOBE Bryant (41) nyota maarufu wa mpira wa kikapu, bingwa wa NBA misimu mitano na mshindi wa tuzo ya Bryant Oscar 2018 na bintiye Gianna Maria Onore (13) wamefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana majira ya asubuhi kwa saa za Marekani katika mji wa Calabasas, vyombo vya habari vimeripoti.

Imeelezwa kuwa Kobe na bintiye ni miongoni mwa watu tisa waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo iliyohusisha helikopta binafsi Sikorsky S-76B ambayo ilianguka na kuwaka moto.

Kifo hicho kimetokea wakati wasanii maarufu duniani wakiwa katika usiku wa tuzo za Grammys 2020 zilizofanyika jana usiku ambapo mtumbuizaji wa kwanza Lizzo alikiri kuwa Bryant amekuwa mchezaji bora wa Los Angeles kwa miaka yote 20 na kusema kuwa usiku huo ni wa Kobe huku mwanadada Alicia keys ambaye alikuwa mshehereshaji wa tuzo hizo alinukuliwa akisema kuwa "Tuna huzuni sana kwa sasa, tumepoteza shujaa" na kwa kumkumbuka aliungana na kundi la Boyz II Men na kuimba wimbo wao "Hard to Say Goodbye" wa mwaka 1991.

Vyombo vya usalama vimeeleza kuwa hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo.

Baadhi ya mashuhuda kutoka wa tukio hilo kutoka Mji wa Las Virgenes wamesema kuwa walisikia sauti kubwa kama bomu na kuona moshi mweusi kilimani huku wengine wakieleza kuwa huenda helikopta hiyo ilikuwa na tatizo la injini.

Kobe ameondoka na bintiye Gianna na kumwacha mkewe Vanessa na watoto wakike watatu ambao ni  Natalia, Capri na Bianca.
Watu wengi wameeleza kusikitishwa na kifo hicho na kusema kuwa Los Angeles, Marekani na dunia kwa ujumla imepoteza mtu muhimu na shujaa sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...