Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha wanaongeza ufanisi na ubora wa kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya, uongozi wa Jiji hilo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe Paul Ntinika wamefanya ziara ya mafunzo jijini Dodoma ili kujionea Maendeleo ya Jiji hilo lililopo Makao Makuu ya Nchi.

Mhe DC Ntinika ameongozana na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo ya Mbeya Mjini, Hassan Mkwawa, Mkurugenzi wa Jiji, Mstahiki Meya na Madiwani na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi.

Akizungumza jijini Dodoma leo, DC Ntinika amesema wameona ni vema wafanye ziara hiyo ya kujifunza namna ambavyo Jiji la Dodoma limepiga hatua kubwa za kimaendeleo ndani ya muda mfupi hasa katika eneo la ukusanyaji wa mapato.

" Mhe DC Katambi tunashukuru kwa kutupokea vizuri, sisi Mbeya tumekua wafuatiliaji wa hatua za maendeleo ambazo Jiji lako la Dodoma imepiga kwa kipindi kifupi hivyo tukaona ni vema tuje tujifunze maana elimu haina mwisho.

Pamoja na kwamba Mbeya ni Jiji kongwe lakini ni wazi Dodoma wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye ukusanyaji wa mapato, upangaji wa Jiji, na namna ambavyo mmekua mkipambana kuthibiti wakwepaji kodi, tunawapongeza sana na tunaimani tutaondoka tukiwa tumepata elimu kubwa," Amesema DC Ntinika.

Amesema licha ya kukaa na wataalamu wa Jiji la Dodoma kwa ajili ya kupata elimu pia watatembelea miradi mikubwa ya kimaendeleo inayojengwa na iliyopo Jiji la Dodoma ikiwemo Stendi ya Kisasa ya Nanenane, Soko kubwa la kimataifa, Stendi ya Malori pamoja na Mji wa kiserikali.

Kwa upande wake DC Katambi amewakaribisha viongozi hao ndani ya Jiji la Dodoma na kuahidi kuwapatia ushirikiano kwa kipindi chote cha ziara yao kwani wanaamini lengo lao wote ni kuwaletea maendeleo watanzania na kukuza uchumi wa Nchi.

" Ndugu zangu hakuna uchoyo katika kujifunza, nyie mmekuja kwetu ila tunaamini kupitia ziara yenu hata sisi pia tutajifunza mengi mazuri ambayo nyie mnayo na sisi hatuna.

Lengo letu ni kumsaidia kazi Rais wetu Dk Magufuli, kuwatumikia wananchi wetu wanaotuamini na zaidi kusukuma mbele maendeleo ya Taifa letu Tanzania," Amesema DC Katambi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe Paul Ntinika baada ya kumaliza mazungumzo yao leo jijini Dodoma.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akizungumza na viongozi na madiwani wa Jiji la Mbeya waliofika jijini Dodoma kwa ajili ya ziara yao ya mafunzo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe Paul Ntinika akizungumza na viongozi wa Jiji la Dodoma, Viongozi wa Jiji la Mbeya kabla ya kuanza ziara yao ya kujifunza mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya Jiji la Dodoma.
 Madiwani kutoka kata mbalimbali za Jiji la Mbeya wakifuatilia mkutano wa pamoja baina yao na viongozi wa Jiji la Dodoma kabla ya kuanza kwa ziara yao ya mafunzo ndani ya Jiji la Dodoma.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...