Na Al-Hassan Muhidin,Globu ya Jamii

Mabaki ya  ya miili yote tisa imepatikana katika eneo la tukio ambalo helikopta iliyokuwa imembeba gwiji wa mpira  wa kikapu Kobe Brayant,mwanae Gianna na wengine saba ilianguka.

Mamlaka katika jiji la Los Angeles nchini Marekani zimesema mabaki ya mwili wa rubani pamoja na mabaki ya miili ya abiria wote nane imepatikana baada ya operesheni  ya kuisaka  miili hiyo kukamilika, hii ikiwa ni baada ya kuwa na Ugumu wa kuifikia eneo ambalo helikopta hiyo iliangukia kutokana na ripoti kudai kuwa chombo hicho kiliangukia eneo la ardhi lenye mteremko mrefu sana.

Hapo awali siku ya jumanne, Alex Villanueva, mmoja wa maafisa wa operesheni hiyo alisema kuwa zoezi hilo lingechukua siku kadhaa kutokana na changamoto ya eneo ambalo helikopta  hio iliangukia, na leo afisa huyo amethibitisha kwamba tayari miili yote imepatikana.

Miili mitatu ilipatikana siku ya jumatatu na baada ya msako zaidi kufanyika mingine sita ikapatikana ambapo mwili wa Brayant ulitambulika kwa njia ya alama za vidole.

Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni John Altobelli Kocha wa timu ya Baseball ya Orange Coast College, mke wake pamoja na mwanao wa kike Alyssa ambaye alikuwa akicheza timu moja ya mpira wa kikapu na mtoto wa Kobe,Gianna.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...