KATIKA kufikia malengo ya kujenga taifa lenye uchumi wa kati ifikapo 2025 Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana (CMSA) imezindua mpango mkakati wa soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kampuni kumi na tano kutoka kada mbalimbali ikiwemo kilimo, fedha na madini ili kuzijengea uelewa, weledi na kufanikisha kutumia soko la fedha hasa soko la hisa ambalo litawasaidia kuendesha biashara zao pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana nchini (CMSA) Nicodemus Mkama amesema,Mkakati huo unaenda sambamba na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano hasa katika kuendeleza kampuni za kati na zinazoibukia katika utekelezaji wa mipango mkakati wa kitaifa.

"Makampuni hayo yakishaingia katika soko la hisa yatawavuta wawekezaji walio katika kipato cha chini na kati, na hii itasaidia sana kuifikia mipango mikakati ya serikali ya kufikia uchumi wakati mwaka 2025" ameeleza Mkama.

Amesema kuwa mkakati huo ni endelevu na amezishauri kampuni kuendelea kujiorodhesha katika soko la hisa na amewashauri wananchi kuendelea kutumia soko la Hisa Dar es Salaam ili kupata fedha za kutekeleza miradi ya kimaendeleo.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa amesema kuwa mkakati huo wa miezi 12 washiriki watapata fursa ya kupata mafunzo ya kibiashara na fursa za kimasoko.

"Kwa miezi sita ya mwanzo washiriki watafundishwa maeneo mbalimbali ya biashara zao, maeneo ya kuwapata wateja, utawala bora pamoja na umuhimu wa kutoa mapato kwa serikali ili yatumike katika kutekeleza miradi mingine ya kimaendeleo" ameeleza.

Pia amesema kuwa kwa miezi mitatu kampuni zilizojitanua zaidi zitazisaidia  kampuni zinazochipukia katika masuala ya kibiashara na miezi mitatu ya mwisho washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu hasa katika utafutaji wa masoko na kutanua biashara.
 Ofisa Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana nchini (CMSA) Nicodemus Mkama,akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar leo wakati akieleza kuzindua mpango mkakati wa soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kampuni kumi na tano kutoka kada mbalimbali ikiwemo kilimo, fedha na madini ili kuzijengea uelewa, weledi na kufanikisha kutumia soko la fedha hasa soko la hisa ambalo litawasaidia kuendesha biashara zao pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Moremi Marwa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari na Wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo,amesema mkakati huo wa miezi 12 washiriki watapata fursa ya kupata mafunzo ya kibiashara na fursa za kimasoko.
Baadhi ya Wadau wakiwa katika majadiliano mara baada ya kuzinduliwa mpango mkakati wa soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kampuni kumi na tano kutoka kada mbalimbali ikiwemo kilimo, fedha na madini ili kuzijengea uelewa, weledi na kufanikisha kutumia soko la fedha hasa soko la hisa ambalo litawasaidia kuendesha biashara zao pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
  Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...