WANAFUNZI wa chuo cha Bahari hapa nchini wakishirikiana na International Peace Youth Group waanzisha matembezi ya amani hapa nchini.

Akizungumza Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Bahari(DMI) Kelvin Rafael wakati wa mkutano wa kuanzisha matembezi ya amani  leo jijini Dar ea Salaam, amesema kuwa amani ni mhimu kwa maendeleo ya nchi na maemdeleo ya mtu mmoja mmoja.

Hivyo wao kama chuo cha Bahari hapa nchini wanaumuhimu mkubwa wa kulinda amani kwani kazi zao nyingi zinafanyika majini ambapo maharamia na wazamiaji wengi hupita majini ili kuharibu amani ya nchi.

Amesema sekta ya bahari kusipokuwa na amani huwa inayumba sana hivyo wanafunzi wa DMI ni mabalozi wa kutunza amani hapaa nchini.

"Vijana tufanye maamuzi ya kulinda amani katika taifa letu la Tanzania, rai kwenu vijana ni kuwa na jukumu la kulinda amani kwaajili ya kutimiza ndoto zako". Amesema Kervin.

Kwa upande wake Meris Ntila amesema elimu ya amani inahitajika kwa kila kijana kwani ndiye mlinzi wa amani wa nchi kwa kipindi cha sasa na baadae.
Hata hivyo ametoa rai kwa serikali kuwahusish vijana katika mikataba ya amani endapo itakuwa ikisainiwa na katika kila mkakati unaowekwa kwaajili ya amani vijana wahusishwe.

Amesema kuwa katika mitaala ya elimu za elimu ya msingi, sekondari na hata vyuo vikuu kuwekwe mtaala wa somo la amani ili kila mwanafinzi kwa kila hatua ajue umhimu wa amani.

Kwa upande wa Mwakilishi wa International Peace  Youth Group hapa nchini, Jeff Kim  amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Pombe John Magufuli kuwaunga mkono katika Matembezi ya amani kwa vijana hapa nchini. 

Mtumuizaji wa nyimbo akiimba wakati wa kuzindua matembezi ya Amani kwa vijana hapa nchini.
  Mwakilishi wa International Peace  Youth Group hapa nchini, Jeff Kim akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Bahari hapa nchini jijini Dar es Salaam, wakati wa kuanzisha matembezi ya amani kwa vijana hapa nchini.
 Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Bahari(DMI) Kelvin Rafael akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Bahari hapa nchini, kuhusu umhimu  wa amani kwa vijana hasa wao kama wanafunzi wanaosoma masula ya maji.

 Balozi wa amani, Meris  Ntila akizungumza juu ya umhimu wa amani kwa wananchi.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Bahari hapa nchini wakiwasikiliza wazungumzaji wakati wa kuanzisha matembezi ya amani hapa nchini kwa vijana. 
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Bahari hapa nchini wakiwasikiliza wazungumzaji wakati wa kuanzisha matembezi ya amani hapa nchini kwa vijana.

Viongozi mbalimbali wakisaini mikataba ya amani hapa nchini wakiwa ni moja wa mabalozi wa amani hapa ncini, katika uanzishwaji wa matemezi ya amani hapanchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...