VICTOR  MASANGU, KISARAWE .
WANANCHI zaidi ya elfu 38 kutoka maeneo ya Wilaya ya  Kigamboni, Ukonga, Bagamoyo, Kibaha pamoja na Wilaya ya Kisarawe kutoka zaidi ya mitaa na vitongoji zaidi ya 62  ambao walikuwa wanateseka kwa kipindi cha muda mrefu kukaa gizani katika makazi yao bila ya kuwa na nishati ya umeme wanatarajia kuondokana na hali hiyo baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa kusambaza umeme Peri- Urban ambao una lengo zaidi  katika maeneo yaliyopo  pembezoni mwa miji.

Hayo yalibainishwa  na Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kisarawe  yenye lengo la kukagua na kutembelea miradi  mbali mbali ya umeme ambapo amemuagiza mkandarasi w kampuni ya Namis kuhakikisha anakamilisha  mradi huo ifikapo mwezi Mei Mwaka huu lengo ikiwa ni kuwafikishia umeme wananchi ili waweze kuutumia katika shughuli mbali mbali za kijiletea maendeleo  ikiwemo kuanzisha ujenzi wa viwanda vidogo vidogo.

Mgalu alisema kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inaboresha miundombinu ya nishati ya umeme sambamba na kusambaza umeme hasa katika maeneo ya vijijini kwa lengo la kuweza kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia nishati ya umeme kupitia miradi mbali mbali ya ujazilishi pamoja na mingine inayosimamiwa na Tanesco pamoja na REA.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwani kutawaondolea kero na usumbufu mkubwa wananchi hususan kwa wale wa maeneo ya vijijini ambao walikuwa wanateseka  kwa kipindi kirefu  kukaa gizani na kutoa pongezi kwa Rais wa awamu ya tano Dk. Dk John Pombe Magufuli kwa kuweza kuboresha sekta ya nishati ya umeme katika maeneo mbali mbali.

“Kukamilika kwa mradi huu sisi kwa upande wetu kama Wilaya ya Kisarawe kutaweza kupunguza changamoto mbali mbali za wananchi ambao walikuwa wanasumbuka kwa kipindi kirefu kutokana na kukosa huduma ya nishati ya umeme kwa hiyo tunapenda kumshuru sana Rais wetu wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli kwa kuweza kutenga fedha ambazo zitaweza kutuletea mabadiliko chanya katika sekya ya umeme, alisema Jokate.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe akizungumza kwa niaba ya madiwani wenzake Hamisi Dikupatile alibainisha kwamba licha ya kuwepo kwa changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika suala zima la upatikanaji wa umeme lakini kwa sasa serikali ya awamu ya tano kupitia mpango wake wa kusambaza umeme  katika maeneo ya vijijini umeweza kuwanufaisha  wananchi wengi na kuwaondolea adha ya kuishi wakiwa gizani.

Alisema kwamba serikali ya awamu ya tano imeweza kuwaletea maendeleo wananchi wa Kisarawe kwa kuwawekea  miundombinu ya nishati ya umeme ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuwainua katika kuendesha shughuli zao mbali mbali za kiuchumi na kuwaondolea wimbi la umasikini na kuwaleta maendeleo.

“Kwa kweli sisi watu wa kisarawe tunashukuru sana kwa Rais wa awamu ya tano Dk.Pombe Magufuli kwa kuweza kutuleta mradi huu wa umeme ambao kwa kweli utakuwa ni mkombozi  mkubwa kw wananchi kwni walikuwa wanapata usumbufu mkubwa kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme hivyo kwa upande wetu ni jambo kubwa sana,”alisema Dikupatile.
 Naibu Waziri wa Nishati wa kati kati Subira Mgalu akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya umeme kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Kisarawe pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa Tanesco, pamoja na REA, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamisi Dipakutile akizungumza jambo kuhusiana na serikali ya awamu ya tano jinsi iliyosaidia kuwaretea mradi wa umeme kwa wananchi wake pamioja na namna utakavyoleta mabadiliko ya kimaendeleo.
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi mbali mbali katika sekta ya nishati ya umeme.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu kulia akiwa ameshikilia cheti maalumu alichopatiwa na ,Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ikiwa ni ishara ya kuonyesha jitihada zake alizozifanya katika kuchangia kampeni ya tokomeza siro ambayo ilianzishwa kwa ajili ya wanafunzi kufanya vizuri katoka masomo yao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...