Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifungua mkutano wa wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM.
Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi akizungumza na waandishi wa wabari wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akipokea jarida maalumu lenye taarifa mbalimbali zinazohusu Shirika la Maendeleo la Japani, (JICA) kutoka kwa mwakilishi Shirika hilo, Naofumi Yamamura
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu( kulia) na Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, Adam Zuberi wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM
Naibu wa Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutosha Shirika la Maendeleo la Japani ( JICA), Wakuu wa Taasisi ya Nishati na Uchumi kutoka Japani, baaadhi ya Viongozi Wakuu wa Wizara na Taasisi zilizochini yake, baada ya Naibu Waziri huyo kufungua mkutano wa wadau hao uliofanyika Jijini DSM.



………………….

Na Zuena Msuya, DSM

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema tayari Serikali imekamilisha mpango wa awali wa kusambaza gesi kwenye Mikoa mitano ili kuhakikisha kuwa Tanzania inatumia rasilimali hiyo inayochimbwa nchini katika kuimarisha uchumi wa viwanda.

Mgalu alisema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM, Januari 17,2020.

Mgalu alisisitiza kuwa mpango huo ni matokeo ya utafiti wa miaka mitatu, uliofanywa na Serikali kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA). Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na Morogoro.

Aidha alieleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mikoa yote Tanzania inapata nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali.

“Tanzania tumegundua gesi asili yenye ujazo wa futi trilioni 57 hii sasa tunaitengenezea mkakati wa matumizi yake, Kwa mijiibu wa takwimu zinaeleza kuwa mpaka sasa gesi asilia inayochiimbwa chini inazalisha Megawati 892.72 sawa na 57 % ya Megawati zote zinazozalishwa.

Aliweka wazi kuwa Gesi Asilia inatumika pia kwenye magari, tumeanza hapa Dar es Salaam ambapo magari takribani 200 yanatumia gesi na miundombinu ya kusambaza gesi hiyo inaendelea kuboreshwa ili kuwasogezea huduma watumiaji, na hii ndio maana hasa ya utafiti huu.

“Gesi asilia inatusaidia pia kutunza mazingira hasa kwenye kupikia ambapo mpaka sasa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesambaza miundombinu ya gesi ya kupikia majumbani katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam na Pwani,” alisisitiza Mgalu.

Kuhusu matumizi ya gesi viwandani Mgalu alisema viwanda zaidi ya 50 vimeunganishwa na gesi asilia. “Huu ni mradi mkubwa Sana utakuwa wa muda mrefu pia hadi kufikia mwaka 2046 tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2017.

Kwa upande wake Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati , Adam Zuberi alisema Tanzania ipo kwenye wakati sahihi hivyo jitihada za makusudi zinafanyika kufikisha gesi asilia kwenye mikoa yote Tanzania. “Tupo katika Muda muafaka wa utafiti huu unaolenga kuhakikisha kwamba Mikoa yote nchini inapata na kutumia gesi asilia kwa njia bora na sahihi,” alisema Zuberi.

Mshauri wa Taasisi ya Nishati na Uchumi kutoka Japan, Kensuke Kanekinyo alisema awamu ya kwanza ya mradi huo imetumia Dola Milioni mbili za Marekani kwa miaka mitatu.

Alisema gharama za mradi wote ni Dola milioni 250 zitakazotumika kupeleka gesi mikoa yote ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...