Mwenyekiti wa EOGESEA, Baraka Mtunga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa shindano la wajasiliamali vijana wanafunzi lilioanzishwa kwaajili ya kutafuta mshindi wa Ujasiliamali katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
 Fatuma Maga akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza shindano la wajasiliamali vijana jijini Dar es Salaam leo.




 Vijana wajasiliamali wakielezea biashara zao kabla ya kumpata mshindi wa shindano la kijana mjasiliamali.
 Mwezeshaji, Miranda Naiman akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpata nshindi wa shindano la kijana mjasiliamali kwa mwaka 2019/2020. 
 Washiriki wa sindano la Mjasiliamali kijana.
Moses Katala, akiwa na cheki ya shilingi milioni moja baada ya kuiuka mshindi wa shindano la mjasiliamali mwanafunzi kijana jijini Dar es Salaam leo.

SERIKALI inaendelea kufarijika pale inapoona taasisi nyingi zisizo za kiserikali zinakuza na kizalisha vijana wengi katika shughuli za ujasiliamali.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya kumpata mshindi wa shindano la kijana mjasiliamali, lililokuwa likiendeshwa kampuni  ya kijasiliamali ya EO.

Mavunde amesema kuwa anatambua kwamba sio vijana wote wataajiliwa katika taasisi za serikali bali wengine wanajikita katika shughuli za kijasiliamali.

"Leo kama serikali tumefurahishwa na taasisi  ambayo imeratibu mashindano haya ambayo tumepata mshindi mmoja, ambaye pia wazo lake la biashara litakwenda kulelewa hadi kufikia matarajio".

Amasema kuwa watashirikiana na wadau kama hawa ili kuhakikisha vijana wengi wakitanzania wanajengewa uwezo ili kufanya kazi za kijasiliamali kwa weredi zaidi.

Washiriki wa mashindano hayo watawawezesha kupata mitaji ili waweze kujiajili moja kwa moja, pia serikali itakuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha wanatimiza azima yao.

Kwa upande wa mshindi wa mashindanobhayo ya kijana mjasiliamali, Moses Katala amesema kuwa changamoto anayokabiliana nayo ni fedha kwaajili ya kuendeleza kampuni yake ya MagoFarm ambayo inazalisha wadudu wanao zalisha protini kwaajili ya kukuzia wanyama wengine.

Hata hivyo Mmoja ya washiriki wa mashindano hayo ambaye anazalisha viungo vya vyakula pamoja na chai, Fatuma Mbaga amesema mashindano hayo yanamfanya awe mwekezaji zaidi kwa sababu pale inapoonyesha watu wanakukubali kwa jambo furani nae anapata moyo wa kufanya vizuri zaidi.

Katika mashindano ya Mwanafunzi mjasiliamali walishiriki wengi kutoka katika vyuo mbalimbali lakini tamati ya mashindano hayo walipata washindi wa tano ambao ni Fatuma Mbaga, Isack Amini, Moses Katala, John Alfred pamoja na Onesmo Stanslaus.

Hata hivyo Moses Katala aliibuka mshindi na kupata mtaji wa shilingi milioni moja na kupewa msimamizi wa biashara yake pamoja na kupata mafunzo zaidi juu ya biashara yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...