Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesaini makubaliano ya Sekta ya Nishati ya mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Waziri ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

Kikao cha makubaliano hayo hufanyika kwa njia ya mtandao(Video conference) kwa kuwakutanisha Mawaziri wa sekta husika kutoka nchi zote wanachama na kujadili masuala yanayohusu sekta ya Nishati katika kila nchi.

Kikao hicho kinatokana taarifa ya Makatibu wakuu wa Wizara husika inayokuwa inazungumzia miradi ama uboreshaji wa sekta ya Nishati katika nchi hizo.

Taarifa hiyo,  huwasilishwa katika ngazi ya Mawaziri kwa hatua zaidi, baada ya makatibu wakuu hao kuafikiana kile walichokikusudia katika nchi zao.

Baada ya majadiliano na kuafikiana na kukubaliana kile walichokikusudia kuhusiana na sekta husika, mawaziri hao huidhinisha na kutia saini   tayari kwa utekelezaji.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...