Pizza Hut Tanzania, imemaliza mwaka 2019 kwa kishindo,kwa kufungua mgahawa wa 8 nchini uliopo katika jengo la Mikocheni Plaza, ambao ulifunguliwa rasmi katika mkesha wa mwaka mpya ikiwa ni wa pili kufunguliwa katika mwezi huo ambapo pia imefungua mgawaha mpya wenye viwago vya kimataifa katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), Desemba 16, 2019.

Mtandao wa migahawa mingine ya Pizza Hut ipo katika maeneo ya Mlimani City, Oysterbay Mall, Mkuki House, Shoppers Plaza, Peugot House na  mjini Arusha katika eneo la maduka ya TFA .

Kampuni ya Dough Works Ltd, ambayo  inamiliki mtandao wa migahawa hiyo inafurahi kufungua mgahawa wa 8 nchini Tanzania na pia inajivunia kupitia uwekezaji huo kuweza kuzalisha ajira zaidi ya 400 “Tunayo furaha kuona biashara yetu inazidi kukua na kuwafikia wananchi wengi na bidhaa zetu za Pizza, zenye viwango vya kimataifa kuzidi kufurahiwa na wateja wetu”. alisema Vikram Desai, Mkurugenzi Mkuu katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa mpya wa Pizza Hut wa Mikocheni Plaza iliohudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mbali na kusherekea kufungua migahawa mipya ya Pizza Hut, Kampuni ya Dough Works Ltd, kwa sasa inaendesha  mtandao wa migahawa 4 ya KFC kuanzia Oktoba 3,mwaka jana.Katika kipindi cha miezi 3 mtandao wa migahawa ya KFC umezidi kukua na kuwa na migahawa 6 baada ya kufunguliwa migahawa mipya miwili mwezi Desemba mwaka jana.Kwa sasa migahawa ya KFC iko katika maeneo ya Kariakoo,Jengo la Diamond Plaza,Mlimani City,Uwanja wa ndege mpya wa JNIA na Mikocheni Plaza, Kampuni inao mpango wa kupanua huduma zake Zaidi kufikia maeneo mengine il ziwafikia wananchi wengi kwa karibu.

Mtandao wa migahawa ipatayo 14 ya KFC na Pizza Hut, inahudumia zaidi ya watu 1,000 ambao hufika kupata chakula pia inatoa huduma za kusambaza chakula chake maarufu cha Pizza na kuku maofisini mpaka majumbani na kampuni imejipanga kupanua huduma zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo katika  mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza. 

Kampuni pia inayo sera ya kusaidia huduma za kijamii kupitia sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii ambapo mwaka huu imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii nchini.

Mkurugenzi wa Dough Works Ltd,Vikram Desai alisema “Tunayo furaha kubwa kuona mtandao wetu  umefungua migahawa 4 katika kipindi kifupi na kuwawezesha wateja wetu kupata huduma zetu kwa urahisi,tutaendelea kupanua huduma zetu katika mikoa mingine na matarajio yetu hadi kufikia mwisho wa mwaka huu tuwe tumefungua mtandao wa migahawa yetu katika miji ya Dodoma na Mwanza ambayo itawezesha watanzania wapatao 250 kupata ajira”,alisema.

Kufunguliwa kwa migahawa ya kisasa ya Pizza Hut&KFC katika eneo moja katika jengo la Mikocheni Plaza, kunatoa fursa kwa wateja kupata huduma bora za chakula hususani Pizza na nyama ya kuku zinazotolewa na migahawa hiyo,inao ukubwa wa eneo la kutosha kuhudumia wateja 90 kwa wakati mmoja,menu za chakula za kidigitali,sehemu nzuri na salama za watoto kuchezea, na mazingira rafiki ya kukutana kwa chakula cha kifamilia na mijumuiko ya sherehe ndogondogo.

Pia migahawa hiyo inauza vyakula mbalimbali vya kuku waliotengenezwa kwa viwango vya kimataifa kwa gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuanzia  kati ya shilingi 7500/ -shilingi 10,000 kiwemo vinywaji vya soda.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akikata utepe  wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa kuuza Pizza  Hut ulioipo katika jengo la Mikocheni Plazza jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works LimIted ,Vikram Desai ( kulia)  na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
 Meneja Mkuu wa Migahawa ya kuuza Pizza Hut Afrika ya KFC,  Ewan Davenport (katikati)  akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limeted ,Vikram Desai ( Kushoto) na Meneja  wa Mgahawa wa Pizza Hut  Mikocheni Emmanuel Sizya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dough Works Limited ,Vikram Desai (kulia) akiongea  kwa wandishi wa Habari hawapo pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Mgahawa w Pizza Hut  na KFC uliopo katika jengo la Mikocheni  Plaza jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni   Meneja Mkuu wa Migahawa ya  Pizza Hut Afrika , Ewan Davenport

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...