Mkurugenzi wa Mkuu wa Taasisi ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadam (NIMR) Profesa
Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari na Maafisa habari wa
Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kuhusiana na mafanikio ya Taasisi hiyo wa kipindi cha miaka minne ya
uwekezaji wa serikali katika vifaa na miundombinu mbalimbali .
Mkurugenzi wa NIMR –Muhimbilli Profesa Sayoki Mfinanga akitoa maelezo
kuhusiana na utafiti wa wanaofanya katika kituo cha Muhimbili na mafanikio yake
katika utoaji wa hudumba bora kwa wananchi.
Msanifu wa Maabara wa NIMR –Muhimbili
Said Omary akitoa maelezo ya utafifi wa kupima
usugu wa vimelea ya kifua kikuu kwa dawa zinazotumika kutibu kifua hatua kwa
hatua pamoja kujua uoteshaji wa vimelea.
Maabara yenye vifaa vya kisasa katika upimaji wa usugu wa vimelea
ya kifua kikuu kwa dawa unaofanywa kwa kuchukua sampuli katika kanda tano.
Maabara ya sampuli NIMR-Muhimbili
Picha pamoja na watendaji wa NIMR –Muhimbili
pamoja Maafisa habari wa Taasisi 17
zilizo chini ya Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) katika miaka mine ya
serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli imeongeza
tafiti kutoka 10 hadi 20 kufikia nwaka 2017.
Tafiti ambazo zimefanyika katika
Taasisi hizo zimeweza kufanya serikali
kubadilisha sera ikiwamo shirika la afya Duniani (WHO) kuunda sera ya kutumia michanganyiko ya
dawa za
kutibu ugonjwa wa mgongo unaosabishwa na fangasi .
Akizungumza na waandishi wa habari
pamoja na timu ya Maafisa Habari wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
hiyo Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa NIMR-Muhimbili katika katika kutekeleza
majukumu yake imefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali kwenye magonjwa yasiyoambukiza
Kifua Kikuu na vimelea vya Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza.
Amesema kuwa kituo cha Muhimbili
kinashirikiana na mpango wa Taifa wa
Kudhibiti Kifua Kikuu katika uboreshaji wa vipima vya maabara ya kitaifa
ya kifua kikuu kwa kupima usugu wa vimelea ya kifua kikuu kwa dawa zinazotumika
kutibu kifua na majibu yake yanatoka ndani siku mbili tofauti na awali majibu
yalikuwa yanatoka kwa kwa miezi miwili.
Profesa Mgaya amesema utafiti mwingine ni ule wa homa ya
uti wa mgongo inayosababishwa na fangasi kwa wagonjwa wenye maambukizi ya
vitusi vya ukimwi ambapo homa hiyo husababisha asilimia 25 kwa wagongwa wenye
VVU.
Amesema kuwa baada ya utafiti huo
kukamilika walifanya tathimini ya mkakati wa tiba wa kupunguza vifo vya
wagonjwa wenye maambukizi ya fangasi na kusababisha homa ya uti wa mgongo kwa
wagonjwa waliothirika na UKIMWI umepunguza vifo vya wastani wa robo tatu ya
kila wagonjwa 100 wanaotibiwa /
Aidha amesema kuwa ugonjwa wa homa ya
uti wa mgongo unasababishwa na fangasi kwa wenye VVU zamani ulikuwa unapunguza
vifo kwa wastani robo moja tu ya kila
wagonjwa 100 wanaotibiwa homa hiyo.
Amesema utafiti wa homa ya uti wa mgongo
unaosababishwa na Fangasi kwa wagonjwa
wa Ukimwi ulifanyika katika nchi za Tanzania na Zambia ulihusisha jumla ya watu
wenye VVU 1999 wenye maambukizi ya fangasi kwenue damu lakini ambao maambukizi
hayo hayajafikia kiwango cha kusababisha homa ya uti wa mgongo utafiti
ulionyesha kupunguza vifo kwa asilimia 30 ukilinganishwa na utaratibu wa zamani
kutumia tiba-kinga kwa waathirika.
Profesa Mgaya amesema Seikali imetoa sh.800 kwa ajili
ya mashine ya kutenheneza dawa
zitokanazo na miti ambapo tafiti zimeshafanyika na wataanza na magonjwa
mawili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...