Na WAMJW- KILIMANJARO, MOSHI

Wananchi wametakiwa kuondoa  hofu, pindi wakikutana na magonjwa ya mlipuko au mhisiwa  mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.

Wito huo umetolewa na Mhandisi Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Francis Mbuya wakati wa kukabidhi majengo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola Mkoani Mwanza na Kilimanjaro.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na jitihada za kuimarisha mikakati ya kudhibiti magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu,hivyo mnapo muhisi mtu ana dalili,toeni taarifa" Amesema Mhandisi Mbuya

Aidha, Amesema kuwa Wizara ya Afya, imekuwa ikitekeleza ujenzi wa miradi mbali mbali nchini ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali mbali mbali za Rufaa nchini pamoja na za kanda lengo ni kupambana na magonjwa aina yoyote ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.

"Miradi hii imejengwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Mawenzi Mkoani Kilimanjaro na Buswelu Mkoani Mwanza inalenga kupambana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu.

Miradi yote miwili (Buswelu Mwanza na Mawenzi Kilimanjaro) imegharimu jumla ya shilingi Bilion 2.2 kutoka Milion 897 iliyotengwa kwa kila mradi, hii ni kutokana na maboresho yaliyofanyika katika miradi hiyo ili kuweza kutoa huduma bora kwa Wananchi.

"Kwa Buswelu mradi umegharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 kutoka Milion 897 iliyotengwa, hii inatokana na sababu ya maboresho kutoka na kutembelewa na Wataalamu mbali mbali kutoka Bank ya Dunia ili kuhakikisha tunakuwa na viwango ambavyo vinakubalika kimataifa, sawa na mradi wa Mawenzi Kilimanjaro", alisema.

Mbali na hayo, Mhandisi Mbuya amewaasa Watumishi wa Hospitali kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vituo hivi katika kipindi chote cha kutoa huduma, ambavyo umeigharimu Serikali pesa nyingi.


Baadhi ya miundombinu ya ndani, katika kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko Buswelu Mwanza.

Moja kati ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kilichomalizika na kukabidhiwa kwa Serikali, kilichopo Mawenzi Kilimanjaro.
Moja kati ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola na Kipindupindu chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1 kilichomalizika na kukabidhiwa kwa Serikali, kilichopo Mawenzi Kilimanjaro.
Kituo cha tiba ya Magonjwa ya mlipuko kilichokabidhiwa kwa Serikali baada ya kumalizika, kilichopo Buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza chenye thamani ya shilingi Bilion 1.1
Mhandisi Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Eng. Francis Mbuya akiteta jambo na Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Dkt. ThAomas Rutachunzibwa baada ya makabidhiano ya kituo cha tiba ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Ebola Buswelu Mwanza.
Mhandisi Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Eng. Francis Mbuya (aliyeinama) pamoja na Wataalamu mbali mbali wa Sekta ya Afya, wakiendelea na ukaguzi katika eneo la kusafishia gari kwa kutumia dawa za kudhibiti maambukizi, baada ya kumshusha mgonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...