Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amekemea vikali tabia ya kuleta ubabaishaji na uchezeaji wa miradi ya kimaendeleo na kutoa saa 12 kurekebisha makosa yote. 

Gavana Shilatu ameyasema hayo leo Jumapili Januari 26, 2020 alipotembelea miradi ya ujenzi na kusisitiza uzembe na ujenzi wa chini ya viwango ni sawa na kuchezea fedha ya umma jambo ambalo halikubaliki. 

“Serikali haina wikiendi wala likizo, leo Jumapili nimepita kwenye miradi mbalimbali ya ujenzi nikabaini kasoro kadhaa, nimewaagiza Mafundi pamoja na Watendaji wazirekebishe mara moja kasoro hizo ndani ya muda usiozidi saa 12, pakikucha Jumatatu Januari 27, 2020 alfajili nisikute kasoro hizo. Nasisitiza tena kasoro zirekebishwe.” Alisisitiza Gavana Shilatu. 

Kasoro alizozibaini Gavana Shilatu ni pamoja na ubovu wa vifaa vya ujenzi pamoja na ujenzi wenye kutilia shaka (ulipuaji kazi) ambao hauendani kabisa na thamani ya fedha tumika. 

Wakati huo huo Gavana Shilatu ameungana na Wananchi wa Kijiji cha Ruvuma kilichopo kata ya Mihambwe kujenga maboma ya vyoo na kusisitiza nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe. 

“Hakuna wa kutujengea Tanzania yetu zaidi ya sisi wenyewe Watanzania. Tuwe na uchungu na uzalendo kwa Taifa letu kwa kuchapa kazi kwa bidii na kumuunga mkono Rais Magufuli anapoijenga Tanzania mpya.” Alisema Gavana Shilatu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...