Naibu Mkuu Wa TAKUKURU Mkoa Wa Morogoro Victor Swella akitoa taarifa ya kazi iliyotekeleawa nataasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia October hadi desemba 2019 kwa  waandishi wa habari.
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO 
TAASISI Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa  TAKUKURU Mkoa Wa Morogoro Imesema Imeweza Kuokoa Kiasi Cha Shilingi Milioni Tisini Na Sita Thelathini Na Tano Elfu Mia Tisa Thelathini Na Mbili Kwa Njia Ya Point Of Sale (POS) Ambazo Zilikua Hazijawasilishwa Kwa Wakati Katika Akaunti Za Mapato Za Halmashauri.
Hayo Yamesemwa  Na Naibu Mkuu Wa TAKUKURU Mkoa Wa Morogoro Victor Swella Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Januari 22, 2020 Akitoa Taarifa Ya Kazi Zilizotekelezwa Na TAKUKURU Katika Kipindi Cha Miezi 3 Kuanzia Octoba Hadi Desemba 2019. 
Swella Amesema Mashauri Yanayohusiana Na Ubadhilifu Wa Makusanyo Kwa Njia Ya POS Yalifanywa Na Watumishi Katika Halmashauri Za Wilaya Za Ulanga Na Kilombero Yamefunguliwa katika mahakama ya za wilaya za ulanga na kilombelo ambapo kesi ECO17/2019 imefunguliwa katika mahakama ya Kilombrlo na  ECO23/2019 katika mahakama ya Ulanga
Katika Ufuatiliaji Wa Maendeleo Amesema Ufuatiliaji Ulifanyika Katika Miradi Inayoendelea Chini Ya Mpango Wa Serikali Za Mitaa Wa Kuendeleza Miji Ambayo Ni Mradi Wa Ujenzi Wa Soko Kuu wenye thamani ya shilingi bilioni kumi na saba milioni mia sita hamsini na tano mia nane thelethini na tatu elfu mia nne na tano na seti sitini na tano(17,655,833,405.65/=).
 Ujenzi Wa  Kituo Cha Daladala Kaloleniwenye thamani ya shilingi milioni sabini na ishirini na nne mia saba sitini na mbili elfu mia tano(724,762,500/=), Mradi Wa Stendi Ya Mafiga wenye thamani ya shilingi bilioni tano milioni mia mbili na arobaini  na saba mia tatu themenini na tano elfu mia tisa arobaini  na senti arobaini na tisa( 5,247,385,940.490
Na mradi mwingine ni ule wa Ujenzi Wa Mtaro Mkubwa Uliopo Eneo La Kikundi wenye thamani ya shilingi milioni mia saba sabini na nne na elfu sita mia tano(774,006,500)
Aidha Takukuru Imetoa Wito Kwa Wagombea Pamoja Na Wapambe Waomwanaoanza Kucheza Rafu Mapema Kwa Kufanya Kampeni Za Chini Kwa Chini Hususani Kuwahonga Wananchi Kwa Lengo La Kuwarubuni Ili Waweze Kuwachagua Kipindi Uchaguzi Mkuu Utakapofika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...