Muonekano wa nje katika banda la Utalii la kwenye maonesho ya Go International Travel Fair nchini Czesh.

Na Augustina Makoye, TTB
KATIKA jitihada zake za kuitangaza Tanzania kwa kituo bora cha utalii Afrika na duniani kwa ujumla Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imebisha hodi katika soko la utalii la Jamhuri ya Czech barani Ulaya. 

Kwa mara ya kwanza TTB kwa kushirikiana na Czech-Tanzania Chamber of Commerce (CTCC) imeshiriki katika onesho la Go International Travel Fair linaloandaliwa na kampuni ya BVV Trade Fairs Brno ya nchini Czech.

Onesho hilo limefanyika  Brno Exhibition Centre mjini Brno, kuanzia tarehe 16  19 Januari, 2020.

Katika onesho hilo Banda la Tanzania lililopambwa kwa utambulisho wake mpya wa TANZANIA Unforgettable lilikuwa kivutio kwa wageni wa mataifa mbalimbali waliotembelea na kushiriki maonesho hayo.

“Onesho hili limetupa fursa ya kujitangaza katika soko hili kwa mara ya kwanza.Tunamshukuru sana Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Possi kwa ushirikiano mkubwa aliotupatia kufanikisha azma yetu ya kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Czech Kupitia onesho hili jipya la Go International Travel Fair," amesema  Afisa Utalii Mkuu, Bi. Doroth Massawe.

Kwa mujibu wa takwimu za utalii za mwaka 2018 Tanzania ilipokea jumla ya watalii 8,506 kutoka Jamhuri ya Czech.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...