Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu (kushoto) akipungia wananchi mara baada ya kuhutubia kwenye Kijiji cha Kibindu Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Januari 21, 2020.

Na mwandishi wetu, CHALINZE.
NAIBU Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu amesema debe tatu za mahindi au kuku tatu zinatosha kuweka umeme ndani ya nyumba.
Mhe.Mgalu ameyasema hayo leo Januari 21, 2020 wakati akizungumza na wanakijiji wa Kibindu Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya kupeleka umeme vijiji vya Kibindu na Talawanda jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
"Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais Dkt.John Pombe Magufuli imedhamiria kufikisha umeme kila kijiji ifikapo Juni 2020.
"Serikali imeshusha gharama za kuweka kutoka bei ya awali hadi shilingi elfu 27,000/-". Alisema Naibu Waziri Mgalu.
 Ameipongeza TANESCO na REA kwa kasi ya  utekelezaji wa mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vijiji hivyo ambapo kwa Kijiji cha Kibindu mradi unatekelezwa kwa umbali wa kilomita 60 wakati kijiji cha Talawanda ni kilomita 26.
"Umeme huu hauchagui nyumba ya nyasi, tope au tofali, zote zinastahili kuwekewa umeme na tunawasihi wananchi mtumie umeme." Alisisitiza Mhe. Naibu Waziri.
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa miongoni mwa wanakijiji wa Kibindu wakimsikiliza Naibu Waziri Mgalu wakati akihutubia.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...