Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuambia upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh.Mil 10 inayowakabili Afisa Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti (26) na mwenzake mtaalamu wa masuala ya Tehama, Theodory Gyan (36), kuwa mwezi ujao kesi hiyo itakapotajwa tena waeleze upelelezi umefikia wapi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Monica Mbogo akisaidiana na Renatus Mkude kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa shauri hilo leo limekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi bado haujakamilika.

Baada kueleza hayo, upande wa utetezi wenye Mawakili 9 ukiongozwa na Alex Mgongolwa umedai kuwa mara ya mwisho upande wa mashtaka ulieleza mahakamani hapo kuwa upelelezi uko katika hatua za mwisho na leo Januari 22,2020 wanasema upelelezi bado wanashindwa kuelewa upelelezi huo umefikia wapi.
Akijibu hoja hizo upande wa mashtaka walidai kuwa, kusema kwamba upelelezi uko katika hatua za mwisho haimaanishi kwamba umekamilika kwani wachunguzi bado wanaendelea na uchunguzi.

Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 5, mwaka huu. Upande wa mashtaka wametakiwa kuja kueleza upelelezi umefikia wapi washitakiwa wamerudishwa gerezani.

Miongoni mwa mashtaka yao inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Februari Mosi, 2019 na Desemba 17, 2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya Tanzania kwa pamoja na watu ambao hawapo mahakamani kwa makusudi walishiriki makosa ya kiuhalifu ya kumiliki programu ya Kompyuta iliyotengenezwa mahususi kufanya kosa la jinai na kuwawezesha kujipatia kiasi cha Sh. Mil 17,354,535.

Pia wanadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Februari mosi, 2019 na Desemba 17, 2019 ndani ya jiji na mkoa  wa Dar es Salaam kwa pamoja washtakiwa hao na mengine ambao hawapo mahakamani walimiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinsi.

Pia wanadaiwa kuwa kati ya Februari Mosi, 2019 na Desemba 17, mwaka huu, ndani ya jiji la Dar es Salaam washtakiwa hao kwa pamoja walijipatia jumla ya Sh. 17,353,535 wakati wakijua mapato hayo yametokana na madharia ya kosa la kushiriki genge la uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...