Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana  na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka
Mnufaika wa MKURABITA, Bw. Heri Nahala akitoa ushuhuda wa namna alivyonufaika na MKURABITA wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kutembelea utekelezaji wa miradi ya MKURABITA katika Halmashauri ya Wilaya ya Njombe .


Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowasili ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kikazi kukagua miradi ya MKURABITA. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Ruth Msafiri.

Na Aaron Mrikaria – Njombe

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amezishauri Halmashauri nchini kushirikiana na Wizara ya ardhi na walengwa wa MKURABITA katika zoezi la kurasimisha rasilimali ardhi za wanyonge ili kuepuka migogoro inayojitokeza.

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe alipokuwa akizungumza na wanufaika wa MKURABITA Wilayani Njombe.

Mhe. Mwanjelwa ametoa maagizo hayo baada ya wananchi kuwasilisha kero zao kuhusu kutokushirikishwa wakati wa zoezi la upimaji ardhi lililofanywa na kampuni binafsi kwa niaba ya Wizara ya Ardhi jambo lililosababisha kumegwa kwa maeneo yao.

“Jambo lililonishtua ni hili la Makampuni kurasimisha ardhi, bila kushirikisha wananchi wa eneo husika hivyo kuna umuhimu mkubwa sasa kwa MKURABITA kuzungumza na Wizara ya Ardhi ili changamoto hii isijitokeza tena kwasababu serikali ni moja” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Mhe. Dkt,. Mwanjelwa amefafanua kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika zoezi la upimaji ardhi utasaidia kuondoa migogoro katika kaya na jamii kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameridhishwa na zoezi la urasimishaji ardhi wilayani humo kutokana na ushuhuda uliotolewa na baadhi ya wanufaika waliofanikiwa kiuchumi baada ya kurasimishiwa ardhi zao ambapo wameweza kuzitumia hatimiliki zao kama dhamana ya kuombea mikopo katika taasisi za fedha.

Katika zoezi la urasimishaji ardhi wilayani humo, jumla ya hatimiliki za kimila elfu kumi na tatu na arobaini na saba zimeshatolewa kwa wanufaika huku wanufaika mianne sitini na tatu wakiwa tayari wamenufaika na mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni mbili.

Akitoa ushuhuda, Mmoja wa Wanufaika wa MKURABITA, Bi. Lucy Mhavile amesema kuwa kabla ya kupata hati miliki za kimila kiwango chake cha kukopa kilikuwa ni shilingi laki mbili tu, lakini mara baada ya kupata hatimiliki ya kimila ameweza kukopa hadi shilingi milioni mia tano na kwamba ameweza kujenga kiwanda kikubwa cha kusaga nafaka Wilayani Njombe.

Dkt. Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya na Njombe ambapo amekagua miradi ya MKURABITA na kusisitiza ushirikiano baina ya wadau wote wanaohusika katika suala la urasimishaji ardhi ili kupunguza umasikini kwa wanufaika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...