Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road imesema kuwa serikali ya awamu ya Tano imewekeza katika ununuzi wa mashine mbalimbali hali iliyofanya kuongezeka kwa utoaji wa huduma mara dufu kwa wagonjwa wanaofika katika taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Julius Mwaisalage amesema kuwa kutokana na uwekezaji wa serikali imeokoa bilioni 15 ya wagonjwa kusafari kupata matibabu nje ya nchi.

Dkt.Mwaisalage amesema kuwa mashine tangu walipozindua mashine katika taasisi hiyo wagonjwa wameongezeka hiyo ni kutokana na vituo vya afya kuimarika kwa kutoa majibu kuhusiana na ugonjwa huo na wanafika wakiwa na alisimia 60 ambao ni hatua za awali katika kansa hiyo.

Amsema moja ya mtambo uliowekezwa wa kutibu kansa umegharimu sh.bilioni 9.5 na kuwa mtambo bora na kufanya Taasisi hiyo kuwa na mashine bora katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Dkt.Mwaisalage amesema serikali inatarajia kununua mshine nyingine ya uchunguzi wa saratani yenye thamani ya sh.bilioni 14 ambapo huduma za katika taasisi zitaendelea kuimarika na kuleta tija ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema katika uwekezaji wa mashine katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road wameweza kuongeza mapato kutoka milioni 500 hadi sh.bilioni 14.77 ikiwa ni pamoja na kujenga mifumo mbalimbali katika taasisi hiyo katika udhibiti wa mapato hayo. “Serikali ya awamu ya Tano katika kupindi cha miaka imefanya maradufu katika uwekezaji ikiwa ni kujali maisha ya wananchi wa katika upatikanaji wa huduma za afya ikiwamo taasisi ya ocean Road”.amesema Mwisalage.
Mtaalam Miozi Tiba Julieth Swai akionesha mashine ya kutibu saratani wakati waandishi habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipofika katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalage akizungumza na waandishi habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Crispin Kahesa akizungumza akitoa maelezo kuhusiana na ujio wa waandishi wa habari habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walifika katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalage akiwa ma timu Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...