Miundombinu ya kisasa,Madaktari Bingwa wapo,mshine ya kila aina za matibabu zinapatikana MOI

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

 Serikali kutokana na uwekezaji wa mashine katika Taasisi  ya Mifupa (MOI) mbalimbali za uchaguzi mifupa kumepunguza wachezaji katika michezo kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Wachezaji walikuwa  wa mpira ndio walikuwa wanaongoza kwenda kutibiwa nje ya nchi lakini sasa wanapata katika Taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Respicius Boniface Amesema kuwa wachezaji hao walikuwa wanakwenda nje baada ya kuumia katika mabega,miguu pamoja na taya za mdomo hivyo mashine zote za kisasa zipo katika Taasisi yetu.

Amesema katika utoaji wa Huduma katika Taasisi hiyo ni wa kimataifa kwani mashine hapo awali hazikuwepo sasa mashine zilizopo ni za hali ya Juu katika viwango vya kimataifa.

Katika uboreshaji wa huduma  kwa wagonjwa watakaokuwa na matatizo ya mishipa ya damu kichwani pamoja na damu kuganda kwenye miguu Taasisi ya Mifupa (MOI) imesema  wagonjwa hapo watatibiwa bila kufanyiwa upasuaji.

Hatua hiyo  ni baada ya serikali kutoa sh bilioni 7.9 katika taasisi hiyo kwaajili ya ujenzi wa Maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo ambapo uwepo wa Maabara hiyo utaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache Afrika zinazotoa huduma hiyo.

Lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo wanaeleza mafanikio waliyoipata katika serikali ya awamu ya tano pamoja na kuelezea mipango yao.

DK.Respicious alisema maboresho hayo yameisaidia MOI kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa ya mifupa,ubongo,uti wa mgongo na mishipa ya fahamu hivyo kuokoa fefha pamoja na maisha ya watanzania wengi.

"Miundombinu hii imesaidia kuongeza idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400 hadi 500 kwa mwezi kufikia wagonjwa 700 hadi 900 kwa mwezi"amesema

Dkt.Boniface amesema  katika kipindi cha miaka minne ya Rais DK.John Magufuli jumla ya wagonjwa 43,200 wamefanyiwa upasuaji ikiwemo ubadilishaji nyonga kwa wagonjwa 900, kubadilisha magoti kwa wagonjwa 870,upasuaji wa mfupa wa kiuno kwa wagonjwa 618 na upasuaji wa ubongo kwa wagonjwa 880,watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 2,070.

Gharama za matibabu haya kwa hapa nchini ni Sh bilioni 16.5 na kama wangepelekwa nje ya nchi sh 54.9 zingetumika hivyo tumeokoa sh.bilioni 38.4.

Aidha Dkt. Boniface akizungumzia huduma  zilizoanzishwa MOI alisema huduma tayari kumeanzishwa huduma ya dawa za usingizi pasipo kulala kwa wagonjwa 250,huduma ya uapasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya mtundu kwa wagonjwa 800.

"Huduma ya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa wagonjwa watano  ,upasuaji wa kunyoosha vibiongo kwa wagonjwa 12 pamoja na upasuaj wa uti wa mgongo kupitia tundu dogo kwa wagonjwa 120"amesema.

Amesema huduma zimewezesha taasisi hiyo kupunguza rufaa za wagonjwa wa nje kwa asilimia 95 ambapo upasuaji unafanyika kwa asilimia 98.Dkt. Boniface amesema Dkt.Magufuli alitoa kiasi cha Sh bilioni 1.5 kwaajili ya ununuzi wa vipandikizi.

Pia alisema MOI kwa kushirikiana na wizara ya afya imejenga chumba maalaumu ambapo wataalamu katika maeneo mbali mbali watatuma picha za X ray na CT scan  ambazo zitasomwa na madaktari bingwa wa radiolojia MOI na majibu kurudishwa kwa muda mfupi.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI) Dkt.Respicious Boniface  na waandishi habari na maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kuhusiana na mafanikio ya Taasisi hiyo kwa kipindi  cha Miaka Minne ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI) akiwa na Timu ya maafisa habari wa Taasisi 17 zilizo chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto walio katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya katika kipindi cha Miaka Minne ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Catharine Sungura akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mafanikio ya Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya kwa kutembelea kwa Namna Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli ilivyowekeza katika sekta ya afya katika utoaji wa Huduma kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...