Na Karama Kenyunko globu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wanne wa mazao ya Misitu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi ikiwemo kukwepa kodi na kutakatisha fedha wa zaidi ya Sh. Mil 155.

Wafanyabiashara hao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Allvay Product Farm, Ebenezer Mmanyi (38),Jumanne Brashi (37), Manish Khattar (38) na Rajesh Velram (52) ambapo wamesomewa makosa yao mbele ya Mahakimu watatu tofauti na kurudishwa rumande kwa sababu mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kukwepa kodi na kutakatisha fedha.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi Ladislaus Komanya amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo  kuwa, kati ya Januari Mosi, na Oktoba 31,2015 katika maeneo tofauti tofauti ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mshtakiwa Ebenezer akiwa na wenzake ambao hawapo mahakamani walitengeneza kundi la uhalifu kwa lengo la kupanga mipango ya uhalifu.

Pia anadaiwa kusafirishia mazao ya misitu yenye thamani ya sh. 6,526000 bila ya kupata kibali cha kusafirishia mazao hayo kutoka kwa Afisa aliyeidhinishwa huku pia anadaiwa kughushi leseni na cheti na kutengeneza nyaraka ya uongo kujaribu kuonesha kwamba nyaraka hizo ni halali na zimetolewa na Afisa aliyeidhinshwa na Zambia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Ebenezer  anadaiwa kughushi leseni ya uzalishaji ( Production license), leseni ya ushirika(Convience license) na pia alitoa nyaraka mbali mbali ikiwemo nyaraka ya uongo ya idhini ya usafirishaji (export permit).


Kosa jingine ni utakatishaji fedha ambapo anadaiwa amelitenda Oktoba 31, 2015 akidaiwa kutakatisha Sh.Mil 6, 526,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la makosa tangulizi.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mfanyabiashara Brashi amesomewa Mashtaka  yake na Wakili wa Serikali, Tuli Helela na kudaiwa kuwa kati ya Januari mosi, 2015 na Oktoba 31, 2015 katika sehemu mbalimbali, mshitakiwa huyo akiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani hapo waliongoza genge la uharifu.

Mstakiwa Brashi anadaiwa kusafirisha mazao ya misitu ambayo ni kontena tano za magogo yenye thamani ya Sh. Milioni 32.6 bila kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka husika. Pia anashtakiwa kwaa shtaka la kukwepa kodi. Helela alidai kuwa tarehe hiyo hiyo katika Jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshitakiwa huyo aliwasilisha nyaraka za uongo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa nia ya kukwepa kodi kiasi cha Sh. Milioni 32.6.

Katika shitaka la mwisho la utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Oktoba 31, 2015 katika jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshitakiwa huyo alijipatia kiasi cha Sh. 32,630,000 wakati akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa tangulizi la ukwepaji kodi.

Baada ya kusoma hati ya mashitaka, Helela alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado  haujakamilika hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hata hivyo Hakimu Chaungu alisema kutokana na kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi,  mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia mshitakiwa huyo dhamana hivyo Brashi amerudishwa rumande.

Wakati huo huo, washitakiwa Khattar na Velram wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde na Silivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ambapo wanakabiliwa na makosa saba ikiwemo kughushi kusafirisha mazao ya Misituz kushindwa kulipa kodi na utakatishaji fedha.

Katika kosa la utakatishaji fedha, inadaiwa walilitenda kati ya Januari 1 na Oktoba 2015 kati ya Tanzania na Zambia kwa pamoja walitakatisha Sh.Milioni 117.48 ikiwa ni mali ya Serikali ya Tanzania huku wakijua zimepatika kwa makosa tangulizi.

Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na washitakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu Uchumi, hivyo wamerudishwa rumande.

Kesi zote zimeahirishwa hadi Februari 12, 202
0 zitakapokuja kwa ajili ya kutajwa





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...