Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Khamisi Kigwangalla picha aliyoiweka leo katika mtandao wake wa Instgramu akiwa mjini Dodoma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii  (Mbunge wa Nzega vijijini),Dkt Khamisi kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika kuhusu  maadui zake wanaomchafua na ambao amedai kuwa wananjama za kupanga kumuua.

 Kupitia ukurasa huo wa Mitandao ya kijamii , Kigwangalla amelitaja gazeti moja nchi kuwa linatumiwa na maadui zake kumfitinisha katika Uongozi wake,na haya ndiyo aliyoaandika kupitia ukurasa wake huo wa Kijamii

"Kuna ukomo kwenye uvumilivu, Uvumilivu ni hekima, Uvumilivu unakuandaa kuwa mtu mwema na bora zaidi mbeleni, Uvumilivu wako usionekane kuwa ni ugoigoi au upuuzi.

"Kuna watu wamenijaribu kwa muda mrefu sana, Kwa kweli sasa wamefanikiwa kunifikisha ukomo wa uvumilivu wangu, naogopa uongo usijegeuka ukweli. Nafahamu watu wema, wachapakazi, watenda haki, wanamageuzi wamewahi kuumizwa kwa sababu ya uvumilivu wao". Ameandika Kigwangalla leo katika ukurasa wake wa Intagramu.

 "Siyo itakuwa ni kukubali uongo ushinde ukweli? Ukiwa waziri wa Maliasili na Utalii ukakuza idadi ya watalii kwa kasi, ukaongeza mchango wa sekta yako kwenye pato la Taifa, ukadhibiti ujangili, ukaufanya utalii ikawa kitu ‘fashionable’, ukazuia ubadhirifu,rushwa,matumizi mabaya ya ofisi, uzembe, badala ya kupendwa na kuungwa mkono watu wanakushambulia".

Amesema kuwa kunawatu wanamuandika kila siku kwenye gazeti lao wanamtuhumu kulipwa ni vya kipuuzi na havina ushahidi wowote, lengo lao ni kumchafua na hii inaonyesha dalili dhahili malengo yao yatimie.

Hata hivyo Kigwangalla ameandika kuwa wanaomchafua wamefanikiwa kusitisha ukomo wake wa vumilivyo ingawa amewapeleka mahakamani.

"Lengo ni kuchafua tu, na hii ni dalili kwamba hawana cha maana cha kutumia kunichafua ili malengo yao yatimie, wangekuwa nacho ningeomba dunia isimame nishuke! Kwa kuwa wao na washirika wao wamenifikisha ukomo wa uvumilivu wangu".

Amesema wanaomuandika wamedanganywa kwa rushwa sasa wanachotakiwa ni kupeleka ushahidi mahakamani kwani yeye ameshawapeleka mahakamani. 

"Anayewapa taarifa za uongo naye tumemjua, aliwahi kusema nilipopata ajali kuwa ‘bora ningekufa’ tu, nilimjua na kumsamehe". Ameandika Kigwangalla katika ukurasa wake wa Intergramu.

Ameandika kuwa waliwahi kupanga mbinu za kumdhuru lakini Mungu alimsimamia, walishindwa kumuua wakati ule, ila kwa sasa hawatoweza kumuangusha kwani anaingia vitani kwa silaha zote.

"Walishindwa kuniua wakati ule, hawatoweza kuniangusha leo. Naingia vitani kwa silaha zote".

Katika Posti nyingine ameandika kuwa Kiasili yeye ni mtoto wa kwanza kwa babu wa kwanza wa baba yake ambaye alikuwa Mtemi au chifu 

"Mababu zangu hawakupewa utemi, walichukua kwa kupigania, hivyo, vita ni asili yangu. Kushinda ni asili yangu. Mimi hupigana vita bila kujali nani atadhurika, iwe mimi ama adui ama collateral yeyote yule, sawa tu. Huwa sijali matokeo ya vita. Aliyenitia kidole jichoni sasa akae sawa".

Hata hivyo Kigwangalla ameandika kuwa hajawahi kuwa daifu wala kuwa mnyonge, hajawahi kukubali kuonewa kukandamizwa wala kunyanyaswa maishani mwake, huwa anapigania haki  na heshima yake.

"Huyu ndiye mimi, hizi nyingine ni tabia tu nilifundishwa na walimwengu na ulimwengu. Asionijua basi afuatilie historia yangu. Twende kazi!" .
Ameandika Kigwangalla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...