Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (aliyevaa miwani) akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Wizara kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto) akisikiliza taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Dkt. Ndumbaro.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Mhe. Mussa Azzan Zungu na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakisikiliza taarifa yaWizara iliyokuwa ikiwasilishwa na mhe. Dkt. Ndumbaro.



****************************


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewasilisha taarifa ya utendaji kazi wake kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi naUsalama na kusema Serikali ina mpango wa kujenga bandari ndogo katika ziwa Tanganyika mpakani mwa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema hayo alipowasilisha taarifa taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya mwezi Juni hadi Desemba 2019 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Mhe. Mwenyekiti, ili kunufaika kiuchumi kupitia DRC, tumepanga kujenga bandari ndogo katika Ziwa Tanganyika na kufungua Ubalozi mdogo katika mji wa Lubumbashi,mji huu uko umbali wa kilomita 3000 kutoka jijini Kinshasa,” alisema Dkt. Ndumbaro.

Amesema ujenzi wa bandari ndogo eneo la mpakani katika Ziwa Tanganyika kutawezesha bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwenda nchini humo kiurahisi kuliko ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wanapitisha biashara zao nchini Zambia hadi kufika nchini DRC.

Aidha amesema Serikali inachukua hatua mbalimbali katika maeneo ya mpaka na nchi hiyo ikiwemo kuhakikisha amani na usalama vinaimarishwa ili wananchi wa pandezote mbili wafanye biashara bila hofu yoyote.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mussa Azzan Zungu imekutana na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kupata taarifa mbalimbali za utendaji wa Wizara.

Mhe. Zungu amesisitiza umuhimu wa Tanzania kushirikiana na DRC katika kuhakikisha amani na usalama vinaimarika hata baada ya Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa (MONUSCO) kumaliza muda wake nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...