Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Mahusiano wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Josephat Kagirwa
akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Fursa za
Mkutano wa Wafanyabiashara wazawa wa Tanzania wanasafirisha bidhaa
kwenda India ambao ATCL imeandaa jukwaa hilo ili kuimarisha biashara kwa
kutumia ndege za ATCL zinazofanya safari zake kutoka Dar es
Salaam-TANZANIA kwenda Mumbai-INDIA.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Mahusiano wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Josephat Kagirwa
akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Fursa
za Mkutano wa Wafanyabiashara wazawa wa Tanzania wanasafirisha bidhaa
kwenda India ambao ATCL imeandaa jukwaa hilo ili kuimarisha biashara kwa
kutumia ndege za ATCL zinazofanya safari zake kutoka Dar es
Salaam-TANZANIA kwenda Mumbai-INDIA.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
na Mahusiano wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Josephat Kagirwa
akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu Fursa za Mkutano wa
Wafanyabiashara wazawa wa Tanzania wanasafirisha bidhaa kwenda India
ambao ATCL imeandaa jukwaa hilo ili kuimarisha biashara kwa kutumia
ndege za ATCL zinazofanya safari zake kutoka Dar es Salaam-TANZANIA
kwenda Mumbai-INDIA.
………………………………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),
limeandaa safari kwa wafanyabiashara wazawa itakayofanyika Machi 4, 2020
kwenda Mumbai India kwa ajili ya kukuza biashara baina ya Tanzania
na nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa
habari Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Mahusiano wa ATCL, Josephat Kagwirwa alisema kuwa safari hiyo itahusisha
wafanyabiashara na abiria wa kawaida na lengo la safari hiyo maalum ni
kukuza biashara kwa wafanyabiashara wa Tanzania kwa kuwaunganisha na
soko la India.
“Katika mkakati wa Biashara wa
ATCL ambao ulianza 2017 ambao utamalizika 2022, tumeandaa safari maalum
kwa wafanyabiashara wazawa nchini kwenda India kwa jukwaa la kibiashara
la siku mbili kuanzaia Machi 5 hadi machi 6,2020, fursa ambayo
itawasaidia wafanyabiashara kupata fursa masoko kwani watatembelea
maeneo mbalimbali ya biashara ikiwemo kituo maalum ambapo bidhaa zote
duniani hufikia na kusambazwa”, alisema Kagirwa.
Kagirwa alisema kuwa tiketi
zitapatikana kwa dola za kimarekani 500 ambayo itahusisha kusafiri
kwenda Mumbai na kurudi Dar es Salaam pamoja na huduma za kutembelea
masoko mbalimbali na dola 700 kwenda na kurudi, huduma za kutembelea
masoko pamoja na malazi.
ATCL imekuwa mdau mkubwa wa
wafanyabiashara katika masoko ya nje kwani mpaka sasa imefanya safari za
kwenda nje takribani mara saba ambazo zimekuwa na tija kubwa.
Serikali ya Awamu ya Tano hadi
sasa imenunua ndege nane kwaajili ya kulifufua shirika la ndege la ATCL
na matunda yake yanaanza kuonekana na miongoni mwake ni hili la wafanya
biashara wa Tanzania kuanza kufaidi uwekezaji huo mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...