……………………………………………………………………………………………….

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa akerwa na ubadhirifu wa fedha katika fidia ya ujenzi wa kituo cha Afya Mikese Morogoro Vijijini.

Dkt. Bashiru amekerwa na ubadhirifu huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha, ambapo fidia ya shilingi milioni 300 ya majengo ya zahanati kutoka kampuni ya ujenzi wa reli ya kisasa kujenga jengo moja pekee ukilinganisha na shilingi milioni 380 zilizokuwa zikisimamiwa na Halmashauri kufanikiwa kujenga majengo saba ya kituo hiko cha afya, ambapo imemlazimu kutoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Loatha Sanare kufuatilia suala hilo.

Dkt. Bashiru ametoa maelekezo hayo leo tarehe 14 Februari, katika mkutano wa ndani wa viongozi wa mashina, Kata, wilaya na mkoa huko Morogoro Vijijini baada ya kutembelea Kituo hiko cha Afya.

“Leo nimeenda Mikese nikaambiwa kuna kituo kimejengwa kama fidia ya Zahanati ambayo imepitiwa na mradi wa treni ya mwendo kasi eti thamani yake milioni 300, lakini majengo karibu saba yalioko pale yaliyojengwa na serikali kwa usimamizi wa Halmashauri ni milioni 380, majengo saba, alafu wao chumba kimoja nilichokiona ni milioni 300.”

Katibu Mkuu ametoa maelekezo kuwa, “Nimeona pale kuna shida, Mkuu wa Mkoa nakuelekeza, uchunguzi ufanyike pale, na waliofanya ubadhirifu huo washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.”

Wakati huo huo Dkt. Bashiru amesisitiza suala la haki kwa wanachi ikiwa ni pamoja na haki ya watoto kupata elimu, malezi na mambo yote yanayohusu maisha ya watu, hivyo amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Ofisi zote za Umma kutenda haki kwa wananchi wote.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amegusia kwa kuonya suala la baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo na kata kabla ya wakati kwa kufanya vikao vya fitina na kuchafuana, hasa kwenye majimbo na kata za CCM.

Amesisitza kuwa, kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya haki, Chama hakitawavumilia wanachama hao.

Katika hatua nyingine, madiwani wawili wa ACT na Chadema Ndg. Khamis Msangule kata ya Tomondo na Juma Manyile kata ya Selembala pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama hivo, wamejivua uanachama wa vyama hivyo na kujiunga na CCM katika mkutano huo.

Katika ziara hiyo, Viongozi mbalimbali wameambatana na Katibu Mkuu wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Ndg. Innocent Kalogeris pamoja na Mkuu wa Mkoa Ndg. Loatha Sanare.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Morogoro katika ziara ya siku 3 ambapo ametembelea wilaya za Kilombero na Morogoro Vijini, ambapo ziara hiyo imelenga katika kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha Chama ngazi za msingi, pamoja na kujenga mahusiano baina ya viongozi wa Chama na serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...