Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imekabidhi msaada wa vyoo matundu kumi vilivyogharimu kiasi cha Tsh. Milioni 15 katika Shule ya Msingi Mloganzila vilivyojengwa kwa lengo la kuunga mkono juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule hiyo ya kuboresha mazingira ya wanafunzi kujisomea.

Akizungumza kabla ya kukadhiwa msaada huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila, Bw. Geofrey Magembe ametaja changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa majengo na upungufu wa vyumba vya madarasa ili kutosheleza idadi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ambao ni zaidi ya wanafunzi 1000.

“Tunaishukuru Hospitali ya Mloganzila kwa kutujengea vyoo hivi ambavyo vitakuwa msaada kwa watoto wetu lakini pamoja na hilo bado shule hii ina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa vitakavyoweza kuchukua idadi ya wanafunzi tulionao ambao ni zaidi ya wanafunzi 1000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru amesema kuwa uongozi wa hospitali unatambua changamoto zinazoikabili shule ya Mloganzila na kuahidi kushirikiana pamoja na wazazi na kamati ya uongozi wa shule hiyo ili kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.

“Natambua ziko changamoto mbalimbali mnazozipata lakini uongozi wa Mloganzila uko pamoja nanyi na tunaomba kwa pamoja wazazi na kamati ya uongozi wa shule hii tushirikiane kwa pamoja ili kupunguza mahitaji ya watoto wetu”

Aidha Prof. Museru amewataka wanafunzi wa shule hiyo kutunza vizuri vyoo hivyo na kuhakikisha wananawa mikono baada ya kutoka chooni ili kujiepusha na magonjwa yatokanayo na uchafu.

“Nawasihi mvitunze na kuvitumia vizuri vyoo na msisahau kunawa mikono mara baada ya kutoka chooni ili kulinda afya zenu mbali na magonjwa yatokanayo na uchafu” amesema Prof. Museru.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Kisarawe, Bi. Zipora Simwanza ameishukuru Hospitali ya Mloganzila kwa ujenzi huo na kuwasihi wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza wakati wa kukabidhi vyoo katika Shule ya Msingi Mloganzila.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mloganzila, Bw. Geofrey Magembe akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaada wa vyoo vilivyojengwa na Hospitali ya MNH-Mloganzila.
Mwanafunzi Frank Richard maarufu kama ‘Ngosha’ na James Ephraim wa Shule ya Msingi Mloganzila wakitumia kichekesho kuishukuru Hospitali ya Mloganzila kwa kuwajenge vyoo.
  Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Kisarawe, Bi. Zipora Simwanza, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof Lawrence wakikata utepe wakati wa kukabidhi matundu 10 ya vyoo.
  Baadhi ya vyoo vilivyokabidhiwa Shule ya Msingi Mloganzila vilivyogharimu Tsh. Milioni 15.
Prof. Museru na Bi. Simwanza wakifungulia maji katika sehemu maalumu ya kunawia mikono mara baada ya kutoka chooni.
Baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Mloganzila na uongozi wa shule ya Mloganzila katika picha ya pamoja mara baada ya kukadhi matundu ya vyoo shuleni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...