Kocha wa Polisi Tanzania Malale Hamsini akizungumza na waandishi wa habari
 Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ushirika Moshi Kilimanjaro
 Afisa Muhamasishaji wa Klabu ya Yangu Antonio Nugaz akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao moja na Timu ya Polisi.


Na.Vero Ignatus Kilimanjaro

Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea kutimua vumbi ambapo Dar Yanga Afrika leo umeendelea kukumbwa na Jinamizi la sare kwa mara tatu mfululizo.

Katika mchezo wao wa leo dhidi ya Polisi Tanzania Yanga katika dakika 45 za mwanzo walionekana kumudu mchezo  huo na kupelekea dakika ya 42 ya mchezo  kipindi cha kwanza Yanga wanajipatia goli la kwanza kupitia jwa  mchezaji wake Tariq Seif jezi nambari 10 mgongoni akaindikia bao la kuongoza hadi Mapumziko.

Kipindi cha pili cha mchezo Polisi tanzania walionekana kufunguka zaidi na kuonekana kushambulia zaidi katika lango la Yanga.

Mnamo dakika ya 71 ya mchezo Polisi Tanzania waliweza kwa mchezaji wake Matheo Anthony Simon jezi namba 32 mgongoni akaindikia Polisi bao la kwanza ambapo muamuzi namba moja Abel Willium kutuka Arusha akalikataa goli hilo.

Katika dakika ya 72 Polisi tanzania kupitia kwa mchezaji wake jezi  namba 17 mgongoni Sixtus Robert Sabilo akaindikia tena Polisi Goli na kubadili matokeo kuwa moja moja.

Nao baadhi ya Mashabiki wa Yanga wameonekana kutofurahishwa na matokeo hayo na kutaka wachezaji kucheza kwenye kiwango.

Naye Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa timu hiyo imecheza mchezo mzuri ingawa makosa madogo madogo yalikuwepo lakini yatafanyiwa kazi kwa kuwa bado kuna ligi inaendelea.

Naye Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz amewataka wana Yanga kuwa watulivu katika kipindi hiki na kuahidi kuwa makocha wapo na makosa madogo madogo yatafanyiwa kazi ili timu iweze kufanya vizuri

Kocha wa Polisi Tanzania Malale Hamsini alisema kuwa anashindwa kuelewa kwanini goli lao limekataliwa wakati ni goli la wazi na halali.

Hata hivyo aliwashukuru mashabiki wa Timu ya Polisi kwa kuujaza Uwanja wa Ushirika na kuwataka kufanya hivyo mara zote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...