Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akiongoza zoezi la kukata utepe, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
 Muonekano wa vitanda na vifaa vya matibabu ndani ya Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akiwa na Naibu balozi kutoka Israel Mhe. Eyal David wakifungua kitambaa, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Muonekana wa Jengo la Kitengo cha matibabu ya magonjwa ya dharura na majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi baada ya tukio uzinduzi wa Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.
…………………………………………..
Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-DOM.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge, leo amezindua Kitengo cha matibabu ya Magonjwa ya Dharura na Majeruhi kanda ya kati katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma.

Katika uzinduzi huo Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amesema kuwa, kitengo hiki ni mkombozi kwa wanachi wa Kanda ya kati hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza matukio ya ajali na magonjwa ya dharura.

“Kitengo hiki ni mkombozi kwa Wanachi wa Kanda hii hasa ukizingatia kuwa ujio wa Serikali hapa Dodoma umechagiza ongezeko na muingiliano wa watu jambo linaloweza kuongeza matukio ya ajali na magonjwa ya dharura jijini na maeneo yanayozunguka jiji la Dodoma,” alisema.

Aliendelea kusema kuwa, Hospitali ya Benjamin Mkapa pamoja na huduma zingine za afya ilianzishwa ili kutoa huduma za Kibingwa, hivyo Serikali inategemea kuona kitengo hiki kikitoa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya dharura na majeruhi.

Aidha, Dkt. Binilith Mahenge amesema, Serikali iliingia makubaliano na Shirika la misaada la Israel (MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa BMH hususan wagonjwa wa dharula na majeruhi,Mbali na hayo amesema kuwa, Shirika hilo limekubali kutoa msaada wa vifaa vya kutoa huduma za dharula na kwa majeruhi na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa juu ya utoaji wa huduma hizo.

“Serikali iliingia makubaliano na Shirika la misaada la Israel (MASHAV- ISRAEL AGENCY FOR INTERNATIONAL DEVELOPMENT COOPERATION) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya zinazotolewa hususan wagonjwa wa dharula na majeruhi, kwa kuboresha eneo la kutolea huduma pamoja na kutoa msaada wa vifaa vya kutoa huduma za dharula na kwa majeruhi. Vilevile kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya” alisema.

Kwa upande mwingine amempongeza Mkurugenzi wa Hospitali ya benjamini mkapa na Watumishi wake wote kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhudumia wananchi wa Kanda ya Kati na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wa Dkt. Alphonce Chandika amesema kuwa, mpaka sasa kitengo hiki cha dharura na majeruhi kimeshahudumia zaidi ya wagonjwa 3,000.

“Kwa Kanda ya Kati, Kitengo hiki kiko hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee. Na mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 3,000 wamepata huduma kutoka katika kitengo hiki,” alisema Dkt. Chandika.

Aidha, Dkt. Chandika amemuomba Naibu Balozi kuendelea kutoa msaada wa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa Benjamin Mkapa ili kuwajengea uwezo zaidi katika kitengo hiki cha dharula na kwenye maeneo mengine ya kibingwa, katika huduma ambazo zinatarajiwa kuanzishwa ikiwemo huduma za matibabu ya moyo, matibabu ya saratani, upandikizaji wa viungo.

Nae Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi ameishukuru amemuomba Naibu balozi Mheshimiwa Eyal David pamoja na madaktari alioambatana nao wasisite kuendelea kuisaidia Hospitali hii pale watakapohitaji msaada toka kwenu, huku akisisitiza kuwa, huu ni mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Serikali ya Israel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...