*****************************

Na. Catherine Sungura-Dodoma

Maambukizi mapya ya ugonjwa wa malaria yamepungua nchini kwa asilimia 27 na hiyo ni kutokana na kuboreka kwa utoaji huduma za mapambano ya ugonjwa huo ukilinganisha na waginjwa 164 kati ya watu 1000 mwaka 2015 hadi wagonjwa 119 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Leonard Subi wakati akitoa taarifa kwa umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania(TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance) waliofika wizara ya afya kufanya uraghibishaji wa kadi ya tathimini ya malaria kwa ajili ya uwajibikaji na utendaji kwa viongozi wa wizara jijini hapa.

Dkt. Subi amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jitahada za viongozi wa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na muhimili wa Bunge katika ushirikiano mzuri na wadau pamoja ma wananchi katika kupambana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa viongozi wa nchi za afrika wanawajibika kwa afya za wananchi na hivyo kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua kwa asilimia 63 kutoka vifo 6,737 mwaka 2015 hadi 2,540 mwaka 2018.

“Ingawa hivi sasa tupo kwenye kudhibiti ila tunalengo la kutokomeza,hivyo tuna imani kwamba tanzania tunao uwezo mkubwa wa kufikia huko kwani kuaniza Mh. Rais Wetu hadi muhimbili kama Bunge nao wako mstari wa mbele kuondosha malaria nchini”.

Aidha, amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kupungua kwa wagonjwa wanaougua malaria kupungua pia hata kwa watoto chini ya miaka mitano vifo vimepungua.

“Tanzania tumeamua kupambana na wadudu dhurifu kuanzia ngazi ya viluilui hadi mbu wapevu waenezao maradhi, hivyo kila mwananchi anawajibu wa kuchukua hatua, hivyo ni vyema tukaungana ili kuiondosha Malaria nchini”.Amesema Dkt. Subi.

Naye Katibu wa TAPAMA Mhe. Raphael Chegeni amesema kuwa msingi wa taifa ni kuwa na afya ,hivyo wanafarijika na afua zinazochukuliwa na wizara ya afya katika kupambana na malaria nchini “Malaria inaua hivyo tunajivunia kuona tanzania inazidi kupambana kutokomeza ugonjwa huu.

Kadi ya tathimini ya malaria ni kitendea kazi cha usimamizi kilichotolewa na wizara ya afya kinachoonyesha takwimu za utendaji wa viashiria vya malaria vilivyopewa kipaumbele katika ngazi ya mikoa na wilaya ambayo inaleta urahisi katika kutambua wapi kuna tatizo ili hatua za kuokoa maisha ziweze kuchukuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...