JESHI la Polisi Mkoani Mbeya leo, Mnamo tarehe 17.02.2020 majira ya saa 03:00 usiku wa kuamkia leo huko eneo la Ilomba, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Gari lori tanker la mafuta lenye namba za usajili T.720 DHV na Tela T.520 CCY likiendeshwa na ABUBAKAR MOHAMED [32] Mkazi wa Dar es Salaam likitokea Dar es Salaam kuelekea nchini Zambia likiwa limebeba mafuta Petrol na Diesel liligongana uso kwa uso na Gari ndogo yenye namba za usajili T.536 DDM aina ya Toyota Carina iliyokuwa inatokea Mbeya Mjini.


Katika ajali hiyo dereva wa gari ndogo T.536 DDM Toyota Carina amejeruhi na anaendelea na matibabu. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa magari yote mawili katika eneo la makazi ya watu. 

Aidha katika ajali hiyo magari yote mawili yameharibika na Tanker la Mafuta liliacha njia na kwenda kugonga maduka ya bidhaa mbalimbali yaliyopo kando kando ya barabara.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama lipo eneo la tukio kuhakikisha mafuta yaliyopo katika gari lililopata ajali yanahamishiwa kwenye gari lingine bila kusababisha madhara yoyote ikiwa ni pamoja na jitihada za kuliinua tanker la mafuta lililoacha njia na kupinduka.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...