Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akionesha zawadi ya fremu ya nembo ya Taifa iliyotengenezwa kwa madini alipotembelea mabanda katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjira.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akiangalia madini ya Tanzanite katika moja ya banda la mjasiriamali wa madini alipotembelea mabanda hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Simon Msanjira.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo katika moja ya banda la mjasiriamali wa madini alipotembelea mabanda hayo katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika JNICC Jijini Dar es Salaam, kulia ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko.
 Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari, 23, 2020.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Madini kutoka Uganda, Mhe. Sara Opendi, akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari, 23, 2020.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akikata utupe kuzindua Cheti cha uhalisia wa madini ya Bati katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania uliofanyika JNICC na kuhudhuriwa na Nchi za Maziwa makuu 11 zinazozalisha madini ambazo zilikutana kujadili mikakati ya kulinda rasilimali hiyo, kulia ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akikabidhi cheti kwa wawakilishi kutoka Nchi 11 za maziwa makuu zinazozalisha madini, mara baada ya kuzindua cheti hicho katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaaam leo Februari 23, 2020.


 Mhadhiri kutoka  Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, Prof. Patrick Lumumba  akiwasilisha mada  katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, Prof.Lumumba aligusia jinsi Afrika inaweza kunufaika na rasilimali ya hiyo, ambapo Tanzania imezindua rasmi cheti cha uhalisia wa madini ya bati.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Prof. Mkenda aligusia jitihada za Serikali katika kulinda rasilimali hiyo.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, Prof. Patrick Lumumba  akijibu swali kutoka kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2020, lililotokana na mada yake, Prof.Lumumba alizungumzia  kuhusu jinsi Afrika inaweza kunufaika na rasilimali ya hiyo, ambapo Tanzania imezindua rasmi cheti cha uhalisia wa madini ya bati, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo.

 Washiri wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipowakuwa akihutubia kufunga mkutano huo JNICC Jijini Dar es Salaam, Februari 23, 2020.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...