Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mjumbe wa Kudumu wa Klabu ya Yanga Thobias Lingalangala ametunukiwa shahada ya uzamivu (PHD) na shirika la lead Impact la nchini Marekani.

Lingalangala amepatiwa shahada hiyo baada ya kujitoa na kuwasaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo kujenga mradi mkubwa wa maji unaohudumia wakazi wa Njombe.

Akizungumza baada ya kutunukiwa Shahada hiyo, Lingalangala amesema kuwa hakujua kama anaweza akapata shahada kutokana na kazi mbalimbali za kijamii alizozifanya.

Amesema, katika Mji wa Njombe ambao ni kwao ameweza kujenga  mradi mkubwa wa maji unaoendana na wa serikali na kwa sasa anafanya usambazaji wa maji kwa wananchi na unaendelea vizuri.

"Nimefanya mambo mengi sana katika jamii, nimejenga mradi huo pia nimeleta mbegu za Maembe za kisasa pamoja na ng'ombe wa kisasa na miradi hiyo inaenda vizuri," amesema

Aidha, amesema anawashukuru sana watanzania wote ikiwemo na shirika la Lead Impact kwa kuona mchango wake kwa jamii na hakutegemea kama siku moja atapata shahada (PDH) kwa kile alichokuwa anakifanya.

Naye Katibu wa Kamati ya Maandalizi kutoka Shirika la Lead Impact  Bishop John Bangenyeka amesema wametoa shahada ya uzamivu za heshima (PHD) kwa watanzania waliojitoa kiroho, utumishi wa umma kama wito kwa wananchi.

Amesema, wametoa shahada hizo kwa watu wa aina mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali waliofanya vizuri katika uongozi wao akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, pia huduma za kiroho pamoja na watu wa kawaida ambao wamejitoa kwa watanzania.

"Tumetoa shahada kwa watu mbalimbali, Lingalangala hakuja hapa kama mtu wa mpira ila kama mtanzania ambaye amejitoa kwa jamii ambapo katika eneo lake ameweza kujenga mradi wa maji, kuwafundisha kilimo cha kisasa na masuala mbalimbali ya maendeleo," amesema

Aidha, amesema Legal Impact wametoa shahada hizi kwa mara ya kwanza kwa wahitimu 29 ambapo kila mmoja ameweza kupatiwa katika sekta tofauti kulingana na kile alichokifanya.

 Mjumbe wa kudumu wa Yanga Thobias Lingalangala akikabidhiwa cheti chake cha Shahada ya Uzamivu (PHD) kutoka Lead Impact kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwa jamii.
 Picha ya watunukiwa Shahada ya uzamivu ya heshima (PHD) baada ya kutunukiwa na Shirika la Lead Impact

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...