Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ametoa onyo kali kwa waongoza utalii wanaofanya shughuli zao Mkoani Arusha baada ya kuhusishwa na usambazaji wa video na picha zinazoonesha uharibifu wa miundombinu katika mamlaka ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Tamko hilo kali limekuja baada ya Gambo kutembelea eneo hilo na kujionea uharibifu wa barabara uliofanywa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

 “Ni marufuku kwa mtu yoyote kusambaza taarifa yoyote kuhusu hifadhi zetu bila kupata kibali cha mamlaka husika, kwetu sisi huu ni uhujumu uchumi kwani tunazitegemea sana hifadhi hizi kwa kuliingizia kipato taifa, kama kuna changamoto yoyote unaiona toa taarifa katika mamlaka husika na si katika mitandao ya kijamii” alisema Gambo.

Aidha Gambo amelitaka jeshi la polisi mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vingine kama TCRA kuhakikisha wanawasaka wale wote waliosambaza video na picha zenye lengo la kuchafua taswira ya hifadhi zetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...