Katibu Mkuu Dkt.Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha afya mazingira (hawapo chuoni).
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha afya mazingira kagemu wakimsikiliza katibu mkuu ambapo anewaahidi kurudisha huduma ya chakula na kufanya ukarabati jiko la chuoni hapo
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiwa kwenyr picha ya pamoja na wanachuo wa mwaka wa tatu wa chuo cha afya ya mazingira kagemu.
***************************
Na. Catherine Sungura-Kagera.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula ameahidi kurudisha chakula kwa wanachuo wote ili kuondoa kupoteza muda wa kujipikia.

Dkt. Chaula ameyasema hayo mara baada ya kukitembelea chuo cha afya mazingira-Kagemu kwenye ziara ya usimamizi shirikishi akishirikiana na TAMISEMI ambao wamefika chuoni hapo kuona mazingira ya chuo hicho ambacho kilipata madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani hapa mwaka 2016.

“Nitaanza ukarabati wa jiko na darasa,ninamwagiza mkuu wa chuo afanye tahimini ili kila mwanafunzi awe na utulivu wa mwili na roho”.
Aidha,Dkt. Chaula amekitaka chuo hicho kuanza mara moja kusafisha eneo la chuo hicho ili waanze kutengeneza matuta kwa ajili ya kulima bustani ambayo itasaidia kupunguza gharama ya kununua mahitaji mengine nje ya nchi.

“Uzalendo unaanzia vyuoni hivyo nitatoa fedha kwa ajili ya vibarua wasafishe eneo la shamba lote na muanze kulima bustani,lazima mjifunze ujasiliamali mkiwa chuoni”.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dkt. Hasan Kawia amesema wamepokea maagizo yote na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwemo tatizo la gari la kuwapeleka mafunzo kwa vitendo wanafunzi hao mipakani
Dkt. Kawia amesema atamfikishia Katibu Tawala wa mkoa suala hilo kwani serikali bado inawahitaji maofisa afya katika kulinda jamii isipate magonjwa hususani yale ya milipuko na vile vile kudhibiti magonjwa kutoka nchi jirani yasiingie nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...