Na Amiri kilagalila,Njombe

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewaelekeza makatibu wa siasa na uenezi ngazi ya kata na wilaya zote mkoani humo, kuhakikisha wanaieleza jamii shughuli za maendeleo zinazoendelea kwenye maeneo yao ikiwa na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya chama.

Wito huo umetolewa na katibu wa siasa na uenezi wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Ndg, Erasto Ngole alipokuyana na viongozi hao katika ofisi za chama wilaya ya Njombe,kupitia ziara ya kikazi anayoifanya mkoani Njombe kwa lengo la kuwafikia makatibu wa siasa na uenezi wa chama ngazi ya kata na wilaya.

Ngole amewataka Viongozi hao kujipanga upya kiutendaji kwa kujituma kuhudumia Chama na jamii kwa kutatua kero za watu na kufuatilia kazi za Serikali ili kufanikisha ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Rais,wabunge na madiwani.

“Kazi yako kama mwenezi ni kuhakikisha unafafanua, kusimamia na kueneza sera za chama kwenye eneo lako, na wauliza ninyi makatibu wenezi huwa mnafanya hivyo au mmeamua kujikita kwenye nyimbo pekee? Badilikeni” Ndg, Erasto Ngole.

Amosi Kusakula katibu wa UVCCM mkoa wa Njombe amesema licha ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali mkoani hapo, ipo miradi mingine ya kitaifa ambayo inaendelea kote nchini hivyo viongozi wa Chama kwenye ngazi husika wanapaswa kuitambua na kuisemea ili wananchi wajue.

“Katika nchi za Afrika,Tanzania tumekuwa miongoni mwa nchi chache zinazopiga hatua kubwa kimaendeleo tunayo miradi mingi inaendelea kutekelezwa kwenye nchi yetu, lakini upande wa huduma ya umeme vijijini Tanzania imekuwa Nchi ya pili Afrika tukiongozwa na Nigeria hii ni hatua kubwa tumepiga” ameeleza Amosi Kusakula.

Seneta Mwaikambo katibu wa jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa Njombe ametoa wito kwa viongozi wa Chama ngazi ya kata kuhakikisha wanadumisha umoja, na ushirikiano kati yao na wanachama ili kujihakikishia ushindi wa kishindo kwenye hchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Katibu wa siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Njombe ndg, Hitla Msola amewataka viongozi wa Chama ngazi ya kata baada ya kupata elimu hiyo ya utendaji kuhakikisha wanaenda kufikisha ujumbe huo kwa viongozi wa ngazi za matawi na mashina ili kuongeza ufanisi wa kazi.

Akiongea kwa niaba ya makatibu wa siasa na uenezi wa CCM ngazi ya Kata walioshiriki kikao hicho Ndg, Solanus Mhagama mwenezi wa kata ya Njombe mjini amesema elimu hiyo imewajengea uwezo na mbinu mpya za kwenda kufanya kazi kwa bidii kwa masilahi mapana ya Chama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...