WAFANYABIASHARA Marijani Msofe maarufu kama Papa Msofe (53) na Fadhil Ibrahim (61) wameunganishwa na wakili wa kujitegemea Abdul Lyana (37) katika kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo mashtaka ya kuratibu genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha na kutakatisha zaidi ya USD, 26,250.

Washtakiwa wote wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Gloria  Mwenda mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi  Augustina Mmbando.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kuomba kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaunganisha washtakiwa wawili na mwenzao katika kesi hiyo ambao walisomewa mashtaka yao wiki  iliyopita

Katika hati ya mashtaka imedaiwa kati ya Januari Mosi na Desemba 30, 2019, jijini Dar es Salaam washtakiwa  wote watatu  waliongoza genge la uhalifu kinyume cha sheria kwa lengo la kujipatia fedha.

Pia imedaiwa siku ya tukio la kwanza washtakiwa wote watatu, walitakatisha zaidi ya Sh. Milioni 60 walizojipatia kwa njia ya udanganyifu ⁹kutoka kwa Yasser Abdelhamad  kwa kijifanya kuwa wangemuuzia tani 25 za madini ya shaba huku wakijua si kweli.

Hata hivyo, washtakiwa hao hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 
Upande wa utetezi ulidai kuwa unaomba muda wa kuwasiliana na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya kujadiliana kuhusu washtakiwa kukiri Mashtaka yao.

Hat hivyo upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na ombi la utetezi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 17, mwaka huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...