Wawakilishi kutoka kiwanda cha Shelly’s Pharmaceutical Tanzania,
wakipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,
Prof.Riziki Shemdoe, baada ya kutangazwa washindi wa kwanza katika programuya KAIZEN kundi la viwanda vikubwa katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindiwa programu hiyo iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa JuliusNyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, akiwa
kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara naKAIZEN mara baada ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa Programu hiyo katika haflailiyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar esSalaam leo Februari 18, 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe, akiwa
kwenye picha ya pamoja na washindi wa tuzo za KAIZEN mara baada ya kukabidhi tuzo hizo katika hafla iliyofanyika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa JuliusNyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof.Riziki Shemdoe akizungumza na washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa program hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.
Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Mhe. Shinichi Goto, akizungumza na washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa programu hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.
Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw.Leo Lyayuka akitoa neno la shukurani kwa washiriki wa programu ya KAIZEN katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa program hiyo ambayo inahusisha viwanda vidogo na vikubwa iliyofanyika katika Kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Februari 18, 2020.
 
Na Eric Msuya - MAELEZO


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka washindi wa shindano la nne la KAIZEN lilopo chini ya usimamizi wa wizara ya Viwanda na Biashara, wakishirikiana na Shirika la Maendeleo kutoka Japani (JICA), kwenda kuitangaza vema Tanzania katika shindano kubwa la KAIZEN litakalofanyika mwezi septemba mwaka huu.

Akizungumza katika halfa ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa shindano hilo lilofanyika leo jijini Dar es Salaam, Prof. Shemdoe amesema kuwepo kwa shindano hilo ni chachu kwa washindi katika kuitangaza Tanzania katika mashindano ya kimataifa ili kufikia lengo la uchumi wa viwanda 2025.

“Niwapongeze sana washindi wa shindano hili la nne la KAIZEN katika falsafa ya kuongeza ubora na ubunifu, tuzo mtakazo pewa mzitumie katika kulitangaza vema taifa letu kwenye shindano kubwa la KAIZEN barani Afrika litakalo fanyika mwezi septemba nchini Afrika ya Kusini” alisema Prof. Shemdoe

Aidha katika hafla hiyo amelipongeza Shirika la Maendeleo la Japan la (JICA) katika kuitekeleza sera ya Mhe. Rais magufuli “Tanzania ya Viwanda” ili kufikia uchumi wa kati kwa ubunifu katika mashindano haya ya KAIZEN

“Niwapongeza sana JICA kwa Mkakati huu mzuri wa kutoa fursa kwa wadau kubadilishana uzoefu na kuhamasishana uendelevu wa tija ili kukuza sekta ya viwanda hapa nchini” alisema Prof.Shemdoe.

Naye Mkurugenzi wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Leo Lyayuka ametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya viwanda na biashara, kujiandaa vema na ubunifu wa hali ya juu na kujituma katika kongamano la KAIZEN kwa Nchi za Bara la Afrika 2021 litakaloanyika hapa Nchini.

“Tanzania tutakuwa wenyeji wa kongamano la KAIZEN katika bara la Afrika mwaka 2021, naomba kutoa rai kwa wadau wote kujiandaa vema kushiriki na kupokea ugeni huu, kujituma kwa dhati na bila kusahau kutumia fursa hizo” alisema Lyayuka

Naye balozi wa Japani hapa Nchini Mhe. Shinichi Goto ameipongeza Serikali ya Tanzania katika sekta ya Biashara kwa kuendelea kuboresha mpango wa Utekelezaji wa kuboresha mfumo udhibiti wa Biashara Nchini (BluePrint)

“Niwapongeze sana kwa kuendelea kuboresha mfumo wa Blueprint, hii ni ishara ya kufikia malengo ya uchumi wa kati wenye viwanda nchini, mfumo huu ni muhimu na ni salama zaidi” alisema Balozi Goto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...