Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta amani katika maeneo yenye migogoro Barani afrika hususani katika Nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuipunguzia Tanzania mzigo wa wakimbizi ulioubeba kwa muda mrefu hivi sasa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani ameyasema hayo katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 33 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaofanyika Addis Ababa Nchini Ethiopia ambapo ameongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ya kunyamazisha silaha (silencing the gun) umekuja wakati muafaka kwa kuwa mapigano na kutokuwepo utulivu katika baadhi ya nchi za Afrika zinachelewesha maendeleo katika Bara hilo.

Ameongeza kuwa endapo Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa zitaongeza nguvu katika kunyamazisha silaha na kukawepo amani na utengamano,ni dhahiri viongozi wataelekeza nguvu kubwa  katika maendeleo endelevu ya wananchi na hivyo kupunguza umasikini katika Bara la Afrika ambalo linaonekana kama Bara lililoghubikwa na migogoro na mapigano.

Mhe. Samia Suluhu Hassani pia ameuahidi Umoja wa Afrika kuwa Tanzania itatekeleza kwa kasi mpango wa Umoja huo katika Mapambano dhidi ya Malaria na kwamba Tanzania imedhamiria kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

Katika Mkutano huo wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wameshuhudia mabadilishano ya uenyekiti ambapo Mwenyekiti anayemaliza muda wake  Mhe.Abdel Fattah el-Sisiambae pia ni Rais wa Misri amekabidhi Uenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini Mhe. Cyrill Ramaphosa ambae anakuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaoendelea Addis Ababa,Ethiopia. Nyuma take ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya nyaraka wakati akishiriki katika Mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaoendelea Addis Ababa,Ethiopia. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete walipokutana katika ukumbi wa mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ukumbi wa Mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa,Ethiopia. Anayeshuhudia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
 Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake Mhe .Abdel Fattah el-Sisi ambae pia ni Rais wa Misri akikabidhi uenyekiti kwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Mhe Cyrill Ramaphosa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni walipokutana katika jengo la Umoja wa Afrika wakati akisubiri kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan Mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...