Mkurugenzi wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa taarifa ya kusitishwa huduma za usafiri wa Treni za Abiria na Mizigo kwa njia ya kati ya Reli.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Sahani.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
KUFUATIA mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini Shirika la Reli Tanzania(TRC) limesitisha huduma za usafiri wa treni za abiria na mizigo kwa njia ya Reli ya kati kutokana na miundombinu yake kuharibika.

Akizungumza na waandishi wa haabari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kuwa uharibifu wa miundombinu hiyo umesababishwa na mafuriko katika maeneo ya Kilosa, Igandu, Dodoma na Makutupora.

"Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali zimesaabisha kufurika kwa mito mikubwa katika njia ya Reli na kuleta uharibifu mkubwa katika njia ya Reli hasa maeneo ya Kilosa Kirosa Morogoro, Gulwe Mpwapwa, Igandu, Zuzu na Makutupora Singida". Amesema Kadogosa.

Amesema Mvua hizo zimeathiri maeneo 26 huku maeneo 10 kati ya hayo yapo katika hali mbaya ambapo tuta la Reli na baadhi ya Makaravati yamezolewa.

Licha ya hivyo Shirika la Reli limechukua juhudi za hali na mali ili kuhakikisha Usafiri wa Reli unaendelea huku wahandisi wa shirika hilo wakiendelea na matengenezo kwenye maeneo ambayo maji yamepungua.

Hata Hivyo Shirika la Reli (TRC) linaomba radhi kwa wadau wa sekta ya miundombinu ya Reli kwa kusimamisha huduma za uchukuzi wa abiria na mizigo hasa ya Dar es Salaam na Dodoma mpaka hali itakapo tengemaa.

Kadogosa amesema kuwa usafiri ukirejea taarifa zitatolewa ili kila mwenye shughuli inayotumia usafiri wa Reli waweze kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo Mwanzo.

Hadi sasa maeneo ambayo yameshaanza kutengenezwa ni maeneo ya kati ya Dodoma na Makutupora.

Hivyo Shirika la Reli linafanya tathimini kwa abiria wote walikuwa wamekata tiketi kwaajili ya Safari ili waweze kuwarudishia nauli zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...