Muonekano wa Kivuko cha MV. PANGANI II baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya wa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilijulikana kama MV. UTETE na kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akiingia kukagua chumba cha kuongozea kivuko cha MV. PANGANI II. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya wa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kikijulikana kama MV. UTETE ambapo kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akitoa maagizo kwa Mkuu wa kivuko cha Pangani Mhandisi Abdulrahman Ameir katikati wakati akikagua injini ya kivuko cha MV. PANGANI II ambacho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya na sasa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na hapo awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi). Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto, Mhandisi Mahangaiko Ngoroma na Mkuu wa kivuko cha Pangani Mhandisi Abdulrahman Ameir wakishuka kutoka kivuko cha MV. PANGANI II. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya wa kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kikijulikana kama MV. UTETE ambapo kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA TANGA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...