Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma ya Airtel Money kwa kushirikiana na Maendeleo Bank Plc pamoja na taasisi ya mfuko wa udhamini wa sekta ya fedha (FSTD)  wamezindua kampeni iliyokwenda kwa jina la "Timiza  Biashara" ambayo imelenga kuwasaidia vikundi vidogo vidogo vya wajasiriamali maarufu Kama vicoba ili kuwawezesha kuweka akiba na kukopa kwa njia ya kidigitali zaidi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Benki Dkt.Ibrahim Mwangalaba amesema kuwa kwa kuungana na Airtel Money benki hiyo imefurahishwa na uzinduzi huo na wanaamini suluhisho la changamoto zinazowakumba  wajasiriamali wadogo zinaenda kutatuliwa.

"Huduma hii imelenga kutimiza biashara na kuleta suluhu ya changamoto ambazo zimekuwa zikivipata vikundi wakati wa kukopa na kuweka akiba" Ameeleza.

Amesema kuwa Timiza Biashara kupitia huduma ya Timiza Vicoba inawezeshwa kwa mtandao wa Airtel pekee kwa Sasa na wateja wanaweza kujiunga kupitia vikundi vya watu watano hadi hamsini kutoka maeneo mbalimbali nchini na kuamua ni siku gani wataweka akiba zao, mkopo wao utakuwa wa muda gani na kuamua ni wakati you watakuwa wakifanya marejesho.

Vilevile amesema kuwa Timiza Vicoba ni huduma inayotumia mfumo wa kidigitali unaowawezesha wanakikundi kuweka akiba na kukopa kidigitali pamoja na kuwasaidia wanakikundi kuendesha shughuli zao huku waliweka akiba na kukopa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya simu ya Airtel Beatrice Singano amesema kuwa malengo ya kuzindua kampeni hiyo ya Timiza Vicoba ni pamoja na kuwajengea watanzania tabia ya kuniwekea akiba hasa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo na hiyo pamoja na kufikisha huduma za kifedha kwa asilimia 80 kwa watanzania ambao hawatumii huduma za kifedha kupitia benki.

" Tutaendelea kuwafikia watanzania wengi na kuwainua pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo na kati juu ya umuhimu wa kutumia mtandao kidigitali kwa kuweka na kukopa, na kwa kuongeza ni kwamba fedha zao zinakuwa sehemu salama zaidi" Ameeleza.

Vilevile Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa wajasiriamali kutoka taasisi ya FSTD Dkt. Peter Kingu amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa na agenda kubwa ya kutoa suluhisho ya changamoto za huduma za kifedha hapa nchini na hasa ni kwa watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki katika maeneo ya vijijini na kwa kupitia kampeni hiyo wananchi wanaweza kunufaika kwa kuweka akiba kidogo kidogo na kukopa kidigitali pasipo kutembelea tawi la benki.

Kingu amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wajasiriamali wadogo na kati katika kutimiza malengo yao ya biashara  na kuwa wafanyabiashara wakubwa zaidi kwa baadaye.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka kampuni ya simu ya Airtel  Beatrice (katikati) Singano akizungumza na wanahabari mara baada ya kuzindua kampeni ya Timiza Biashara kupitia huduma ya Timiza Vicoba na kusema kuwa wataendelea kuwafikia watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kufikia malengo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo Cha uwezeshaji wa wajasiriamali kutoka taasisi ya FSTD Dkt. Peter Kingu (kulia)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Timiza Biashara kupitia huduma ya Timiza Vicoba ambapo amewashauri wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kutumia fursa hiyo ili wakuze biashara zao, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank Plc, Dkt. Ibrahim Mwangalaba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Timiza Biashara kupitia huduma ya Timiza Vicoba na kusema kuwa huduma hiyo italeta suluhu ya changamoto ambazo zimekuwa zikizikumba vikundi vya wajasiriamali wakati wa kuweka na kukopa leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...