NUNGWI, ZANZIBAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu mwingine.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua kituo cha utalii Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kisiwani Zanzibar, huku akiwataka watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kisheria na kufuata maelekezo ya Jeshi hilo.

Kuhusu Corona IGP SIRRO ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kiserikalipamoja na wataalamu wa masuala ya afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis, amesema kuwa, mkoa huo unaidadi kubwa za hoteli za kitalii na kwamba ujenzi wa kituo hicho cha Polisi utasaidia zaidi katika kukabiliana na kuzuia uhalifu.

Ujenzi wa kituo hicho ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 64 zilizotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa utalii visiwani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...