…………………………………………………………………..

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate imepata Nafasi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Karate Japani mwezi October Mwaka huu.

Mashindano hayo ya Karate ya Dunia huwa yanafanyika kila baada ya Miaka 3,na kwa mwaka huu Tanzania pia imepata nafasi ya Kipekee kwa kutoa Jaji wa michuano hiyo ambaye ni (Sensei)Jerome Mhagama.

Jerome Muhagama ambaye Pia ni Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania amezungumzia Juu ya nafasi hiyo iliyopata nchi ya Tanzania.

Haya ni mashindano ya 15 ya Dunia Tangu kuanzishwa kwake,na Tanzania imewahi kushirikiki mara Mbili katika mashindano hayo. Kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mashindano hayo yaliyofanyika Nchini Tailand,Tanzania Ilipeleka mchezaji mmoja ambaye alifika katika hatua ya 16 Bora.

Mwaka 2014 Katika mashindano yaliyofanyika Japan Tanzania Ilishiriki katika mashindano hayo kwa Kupeleka Jaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...